Mbio za kuruka vihunzi au (hurdles), ni mbio ambazo zimeadimika kama siyo kupotea kwa kasi hapa nchini pengine hata kusahaulika kabisa katika masikio ya walio wengi.
Mbio hizi za vihunzi ambazo huwa na vizuizi vya
chuma, mshiriki huruhusiwa kukimbia kuanzia umri wa miaka 15 na
kuendelea na huwa na tofauti kati ya wanawake na wanaume.
Katika mbio hizi kwa wanawake huwa na mbio zao na
wanaume pia huwa na mbio zao, ambapo wanawake huruka mita 3.5 huku
wanaume wakiruka mita 4 kamili na kila safu au barabara ya kukimbilia
ambazo ni njia nane kila mchezaji hupaswa kuruka vihunzi 6 mpaka mwisho.
Idadi kamili ya vihunzi ambavyo hupangwa uwanjani
kabla ya kukimbia huwa ni 40 ambavyo hupangwa katika njia nane za
kukimbilia huku ikitegemea ukubwa wa uwanja na mistari iliyochorwa.
Umbali wa kila kihunzi hadi kihunzi ni mita 7 kwa
pande zote mbili yaani kwa upande wa wanaume na wanawake, lakini katika
mchezo huu kinacholalamikiwa zaidi ni gharama za vifaa vya mbio hizi.
Vifaa vya mchezo huu ni adimu na havipatikani kwa
urahisi, hapa nchini vifaa vya mchezo huu vipo kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam pamoja na Chuo cha Michezo kilichopo mkoani Arusha.
Vihunzi ni vyuma vigumu sana hivyo endapo mkimbiaji atakosa umakini kwa kugonga maeneo ya magoti anaweza kupata kilema.
Mbio hizi za kuruka vihunzi ni tofauti na mbio za
kawaida kwa kuwa katika ukimbiaji wa mbio hizi nguvu ya ziada
inahitajika kutokana na mpangilio wa vihunzi anavyowekewa mkimbiaji
wakati wa kukimbia.
Mkimbiaji wa mbio hizi anapaswa kuepuka na vyakula
vyenye mafuta mengi kama chips, samli, karanga na vingine vingi ila
anashauriwa kutumia mboga mboga, matunda kama machungwa kwa wingi,
mapapai, matikiti pamoja na kunywa maji mengi mara kwa mara bila kusahau
mazoezi ya mara kwa mara
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia