RADIO 5 YAMKABIDHI MTANGAZAJI WAKE PIKIPIKI
Mkurugenzi wa Tan
Communication Media inayo miliki kituo cha Radio 5 chenye makao yake
makuu jijini Arusha Bw Robert Francis (kulia) akimkabidhi Pikipiki
Mfanyakazi Bora wa Kituo hicho Semiyo Sonyo.
Mkurugenzi wa Tan
Communication Media inayo miliki kituo cha Radio 5 chenye makao yake
makuu jijini Arusha Bw Robert Francis Amewataka watangazaji na
wanahabari wanaofanya kazi katika vituo vya Radio na Televisheni hapa
nchini kuzingatia weledi wa kitaaluma wanapofanya shughuli zao za kila
siku ili kusaidia jamii ya kitanzania kukabiliana na changamoto katika
kipindi hiki ambacho dunia inabebwa na utandawazi.
Akikabidhi pikipiki kwa
mtangazaji bora wa kipindi cha usiku cha LOVE CUTTS kinacho rushwa Radio
5 katika Hafla fupi iliyofanyika jijini Arusha, Mkurugenzi Robert
amesema vyombo vya habari vya kielectonic yaani Televisheni,Radio, na
mitandao ya kijamii vinafikia watu kwa haraka zaidi na kwa unafuu wa
gharama kuliko machapisho na kwamba vikitumika bila miiko ,weledi na
kuzingatia kanuni za kitaaluma vinaweza kuwa sehemu ya tatizo badala ya
kuwa vyombo vya kusukuma kasi ya maendeleo.
Katika tafrija hiyo Mtangazaji
Semio Sonyo amekabidhiwa pikipiki ikiwa ni sehemu ya motisha zinazo
tolewa na kituo cha Radio five kwa wafanyakazi wake waofanya vizuri
katika majukumu yao.
Semio Sonyo akijaribu pikipiki aliyokabidhiwa na mkurugenzi wa Tan Communication Media,bwana Robert Francis
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia