|
Joan Rivers Joan Rivers amefanyiwa upasuaji mara nyingi kurekebisha sura yake.Amesema kwa sasa hahitaji kufanyiwa upasuaji tena! |
|
Madonna Madonna
amefanya marekebisho katika uso wake. Kaka yake Madonna alikubali kuwa
Madonna alifanya upasuaji wa kunyanyua ngozi ya uso wake kiasi kumfanya
yeye(kaka yake),kushindwa kumtambua Madonna. |
|
Mel B
Nyota
wa iliyokuwa Spice Girls Mel B ana umbo lenye mvuto.Nyota huyu
alifanyiwa upasuaji kuongeza ukubwa wa matiti yake.Uongezwaji wa matiti
ulimletea matatizo na kuamua yaondolewe. Pamoja na hivyo Mel B bado
anaonekana ni mrembo |
|
Michael Jackson Mengi yaliandikwa kuhusu marekebisho
yaliyofanyika katika uso na ngozi ya nyota huyu.Inasadikiwa kuwa Michael
alifanyiwa upasuaji mara kadhaa kupunguza ukubwa wa pua yake!Rangi ya
ngozi yake nayo ilibadilika kama picha ionyeshavyo!
|
|
Tina Turner Tina
Turner alifanyiwa upasuaji wa pua ambapo mwenyewe amekubali hilo.Hiyo
ilikuwa ni kutokana na na manyanyaso na kipigo alichokuwaakipata kutoka
kwa mumewe Ike na kusababisha mfupa wa pua kuvunjika na hivyo kupelekea
yeye kufanyiwa upasuaji huo.Kuna habari za chini chini kuwa amefanyiwa
upasuaji wa kunyanyua ngozi ya uso wake kwasababu licha ya kuwa na umri
mkubwa Tina anaoneka mrembo bado! |
|
Queen Latifah Kutokana
na maimivu ya mgongo na mabega aliyokuwa nayo Queen Latifah,ilimpelekea
afanyiwe upasuaji kupunguza ukubwa wa matiti yake hivyo Queen Latifah
alifanyiwa upasuaji si kwaajili ya sababu za urembo! |
|
Jermaine Jackson Siyo
siri kuwa Jermaine Jackson amefanyiwa upasuaji wa kurekebisha pua na
marekebisho katika ngozi yake.Habari zake zimekuwa zikiandikwa sehemu
tofauti kwa muda sasa. |
Idadi ya wasanii na
matajiri waliofanya urekebishaji wa sura na ngozi zao ni kubwa na hawa
ambao Sophie Mbeyu Blog imewatoa leo ni baadhi tu.Jamani,pesa
zisitufanye tukamkufuru Mungu kwa kuikosoa kazi yake.Haya,ona wengine
wameongeza maziwa,mara yanawasumbua wanaamua kuyatoa.Wengine ngozi
zimebadilika kiasi ambacho unaweza kumpita mtu!
Tumeona watu wakijichubua
na kuwa katika mwonekano wa kutatiza.Tumeona wengine wakiongeza makalio
na kupata maumbo ya kutisha.Tujifunze kwa waliopata madhara na
marekebisho ya miili yao na tufurahie kuishi katika mwonekano Mungu
aliotupa!