Muoenekano
wa ujenzi wa mradi wa daraja la Kigamboni katika awamu ya kwanza ukiwa
umekamilika kwa asilimia 47, katika mradi huo. Ujenzi huo utagharimu
jumla ya Sh. Bilioni 214,kati ya fedha hizo asilimia 60 zimetolewa na
Shirika la Hifadhi ya Mfuko wa Jamii (NSSF). Picha hii imepigwa jana
wakati Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (hayupo pichani) alipofanya
ziara ya siku moja ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi ya
Miundombinu hiyo ya jijini Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na ujenzi wa
daraji hili.
Picha ya Daraja hilo kama ilivyopigwa kutoka juu inavyoonekana.
Ujenzi wa barabara unaoendelea katika barabara ya Davis Corner- Vituka - Jet Corner.
Ujenzi
wa baadhi ya Vituo vya mradi wa Mabasi ya mwendo kasi (DART) barabara
ya Morogoro, eneo la Ubungo,Mwembechai na Jangwani vikiendelea.
Sehemu ya muonekano wa kituo cha mabasi ya mwendo kasi eneo la Kigamboni.
Waziri
wa Ujenzi Dkt, John Magufuli, (mwenye kofia ya pama) akiongea na
Diwani wa kata ya Mwenge Dkt. Julian Bujugo (aliemshika begani) wakati
ya ziara yake .
Picha
ya Pamoja kati ya Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli pamoja na
viongozi waliokuwa katika ziara yake. Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia