mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe kulia akiwa na mlemavu wa ngozi (ALBINO) mara baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni za ubunge
Na Matukiodaima Blog Ludewa
WAKATI wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) kesho wanashiriki zoezi la kupiga kura za maoni kuwapata madiwani na wagombea watakao gombea kwa CCM ,mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amewashukuru wanachama wa CCM katika jimbo hilo kwa kuonyeha imani kubwa kwake ukilinganisha na wagombea wenzake wawili na kuwa hadi sasa anauhakika mkubwa wa kushinda tena ila ushindi utakaompa heshima ni ule wa kupata kura zote na wenzake kuambulia patupu
Filikunjombe aliyasema hayo wakati wa mkutano wa kujinadi kwa wagombea wa nafasi ya ubunge katioka kata ya Ludewa mjini ,kuwa hadi sasa kutokana na mapokeo ya wananchi na wana CCM kote walikopata kupita kwenye kata 26 za jimbo hilo la Ludewa wamekuwa wakitamka bayana kuwa kura zote kwake hivyo kuwaomba wana CCM kwa umoja wao kumpa moyo zaidi wa kuwatumikia tena kwa kuhakikisha wanampatia kura zote za ndio.
Alisema kwa kauli zao wagombea wenzake wawili waliojitokeza wanaeleza bila kuficha kuwa wametumwa na watu ambao aliwaondoa bungeni kutokana na vitendo vyao vya ufisadi ili waje Ludewa kugombea ubunge kwa ajili ya kulipa kisasi kwa kumtoa jambo ambalo hadi sasa limegonga mwamba kutokana na wananchi na wana CCM Ludewa kuliona hilo.
"Niliifanya kazi ile ya kupambana na mafisadi bungeni kwa faida ya wananchi wa Ludewa na watanzania kwa ujumla ila nashangazwa kuona leo wana Ludewa wachache wanakubali kutumika na mafisadi hao kutumwa kuja kunitoa ubunge kweli ni aibu kubwa kwa kazi kubwa ambayo mimi nimeifanya katika jimbo la Ludewa sikutegemea kupata mpinzani tena ndani ya chama changu.....ila naomba sana wana Ludewa tuungane katika vita hii ya maendeleo na kupinga ufisadi kwa kuwanyima kura hawa "
Alisema kuwa wilaya ya Luudewa itajengwa na wana Ludewa kwa kushirikiana na yeye kama mbunge wao na sio wale wanaotumika kuwadanganya wananchi wa Ludewa hata kupinga kazi kubwa iliyofanyika kwa kipindi kifupi cha miaka mitano .
Filikunjombe alisema kuwa hawezi kusema kuwa amemaliza changamoto zote za wilaya hiyo ya Ludewa kwani kama atasema hivyo atakuwa anawadanganya wananchi wake na kuwa pamoja na kuwa amefanya mengi ila hajamaliza changamoto zote za jimbo la Ludewa hivyo iwapo watampa tena nafasi hiyo ua ubunge atahakikisha anaendelea kupunguza changamoto zilizobaki.
" nimefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo jimbo la Ludewa ila nitakuwa nadanganya kama nitasema nimemaliza changamoto zote pia hata wabunge wenzangu walifanya kulingana na wakati ule na kila mmoja a namchango wake katika maendeleo ya Ludewa .....ninachowaomba wananchi mtupime wagombea kwa kazi tulizofanya msitupime kwa maneneo kwangu mimi ni kazi zaidi maneno kidogo"
Hata hivyo alisema iwapo wananchi wa kata ya Ludewa watamchagua kuwa mbunge kwa kura za kishindo atahakikisha kero ya maji anaanza kuitatua kabla ya serikali kuanza kufanya hivyo kwani kati ya changamoto kubwa kwa mji wa Ludewa ni pamoja na maji .
Pia aliwataka wananchi kupuuza uongo unaosambazwa na wagombea hao kuwa vikao vya juu vya chama vimepanga kukata jina lake baada ya kushindwa na kudai kuwa huo ni upotoshaji na kuwa CCm ni chama makini na hakuna mtu wa kukatwa iwapo ametekeleza sera vema za chama.
Huku mgombea injinia Zephania Chaula akiwaomba wananchi hao kumchagua kuwa mbunge kwani tayari ameahidiwa na na mwenyekiti wa DP mchungaji Christopher Mtikila na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kabla ya kuangushwa na mbunge filikunjombe mwaka 2005 Prof Raphael Mwalyosi kuwa watamsaidia kufanya kazi pamoja .
Chaula ambae alipingwa vikali katika mkutano huo kiasi cha kuzomewa baada ya kudai moja kati ya kazi aliyoifanya ni kuanzisha mfereji wa umwagiliaji kata ya Ruhuhu baada ya mkazi wa kata hiyo aliyekuwepo mkutanoni hapo kunyosha mkono na kumpinga kuwa hakuna mradi huo ni uongo na kuwa wao wanamtegemea mbunge wao Filikunjombe ambae amefanya mengi kwenye kata hiyo.
Wakagti Injinia Chaula ambae siku za hivi karibuni aliambulia kura 11 katika nafasi ya ujumbe wa NEC akipingwa vikali mkutanoni hapo mgombea Kepten (mstaafu) Jacob Mpangala akijikuta katika wakati mgumu kufuatia mbunge Filikunjombe kuwasilisha vielelezo sahihi mbele ya viongozi wa chama na kugawa kwa wananchi hao viinavyoonyesha mgombea huyo anavyodanganya wananchi kuwa alistaafu kazi wakati kuna barua ya kufukuzwa kwake kazi kutoka TAMISEMI.
Filikunjombe alifikia hatua hiyo ya kukabidhi ushahidi huo kwa chama baada ya kauli ya vitisho ya mgombea huyo Mpangala kumtaka aonyeshe hadharani ushahidi unaoonyesha kufukuzwa kakwe kazi kabla ya kuchukua hatua .