Ticker

6/recent/ticker-posts

MLEZI WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM BAYI AJITOSA KUWANIA UBUNGE

 Mlezi wa Jumuiya ya wazazi  wa CCM wilaya ya bahi  Hebron Kipiko (Mr.Kipiko) katika picha


Mlezi wa Jumuiya ya wazazi  wa CCM wilaya ya bahi  Hebron Kipiko (Mr.Kipiko)  ametangaza rasmi nia ya kugombea ubunge wa jimbo la Bahi lililopo mkoani Dodoma  na kusema kuwa anaamini  anauwezo wa kutekeleza kero na matatizo mbalimbali ya nao wakabili wananachi wa jimbo hilo.

Akizungumza na Libeneke la kaskazini blog ,  amesema kuwa ameona mambo mengi na matatizo mengi yanayo wakabili wananchi wa jimbo lake na pia   huu ndio wakati muafa kwake kuwatumiakia wana Bahi.

Kipiko alisema kuwa , wana wa  bahi  wananafasi sasa ya kuandika historia  ya aina yake kumchagu yeye kama mgombea kwani wameona tu baadhi ya mambo ambayo ameyafanya wakati alivyokuwa mlezi wa jumuiya ya wazazi wa ccm wilaya,  pia ni mmoja wa mzazi  mchapakazi mwenye uwezo wa kutetea na kuwasilisha hoja za kuleta maslahi kwa  Bahi  na taifa.

“Huu ni wakati wa wananchi wa Bahi  kuandika historia ya aina yake, sit u kwa kumchagua kwa ajili ya  kuwaongoza bali  ni Mzazi  mwenye uwezo wa kutetea hoja na maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla,”alisema Kipiko.

Kipiko  amekuwa ni mwananchi wa kwanza  kujitokeza kugombea jimbo la Bayi na ni mwana CCM wa  wa kwanza kujitokeza kuomba ridhaa ya chama kuteuliwa kugombea Ubunge kwa tiketi ya chama hicho.

Aidha aliainisha baadhi ya mambo ambayo atayatekeleza iwapo atapewa ridhaa  ndani ya chama na ndani ya jimbo kuongoza ,ambapo alisema jambo la kwanza alisema kuwa kumekuwa na tatizo la maji sana katika jimbo lake kitu ambacho ataanza nacho pindi tu atapewa ridhaa ,atajenga Zahanati ,shule ,atatengeneza barabara pamoja na kujenga hospitali

Post a Comment

0 Comments