Huu ndio msikiti wa Masjid Fisabillah ya Mlamleni uliopo Kijiji cha Kimbangulile, Wilaya ya Mkuranga , Mkoa wa
Pwani.
Ujenzi wa Msikiti ukiwa umeanza.
Hivi ndivyo ujenzi ulipofikia katika ujenzi huo na bado fedha zinahitajika kwaajili ya kuendelea.
***********
Tunamshukuru M/Mungu kwa
Pumzi anayo endelea kutupa.
Ufuatao ni Mrejesho wa
Michango yenu ya Ujenzi wa Msikiti wa Masjid Fisabillah ya Mlamleni , Mkoa wa
Pwani , Wilaya ya Mkuranga , Kijiji cha Kimbangulile.
Ikumbukwe kupitia Blogs na
Mitandao ya Kijamii tulitoa Wito na Tangazo la watu kujitolea Vifaa vya Ujenzi
wa Msikiti ambao ulikuwa katika hali ya Manyasi .
Tunashukuru M/Mungu
mwitikio ulikuwa Mzuri , Ndani ya Miezi miwili tumeweza kukusanya Fedha Tshs 4,352,022/=
kwa Ajili ya Ujenzi huu wa Msikiti .
Kupitia Pesa hizi tuliweza
Andaa Maandalizi ya Kiwanja , tulinunua Tofali , Cement na baadhi ya Vifaa
vichache vya Kuanzia Ujenzi wa Msikiti huu.
Alhamdullilah tulianza
kuchimba Msingi na kulaza Tofali 2000 , na hali Mnayo iona kwa Picha ni
kutokana na Juhudi zetu na Nguvu zetu .
Naomba itambulike kutokana
na Gharama kubwa ambayo itatumika katika kuhitimisha Ujenzi tupo katika
Mazungumzo na Moja katika Shirika la Misaada ya Kidini lipate kuhitimisha pale tulipo fikia wakati ambao tukiwa katika
hali ya kusubiria kufanya Majukumu
mengine ya Kimaendeleo .
Nawashukuru wote mlio
shiriki na Mtakao penda kushiriki zaidi katika PROJECT hizi za kheri .
Nichukue fursa hii vilevile
kuwatakia Kheri ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambao unatuacha na pia Niwatakie
Sikukuu Njema ya Eid el Fitri .
Tunakaribisha Zaidi
Michango yenu kukamilika kwa hili ndio Mwanzo wa Mengine ,
Kwa Uchambuzi zaidi Ungana
nami katika Mtandao wa Facebook : Kijana wa Kiislam Dsm .
WASILISHA
MCHANGO WAKO KUPITIA NAMBA ZIFUATAZO .
+255715800772
+255673800772
+255689604780
Hakikisha
Jina kabla ya kutuma GHALIB MONERO.
+254725113783
M- pesa KENYA (Ali Hamis)
Waliopo
Uingereza wawasiliane Na +447460340642
Au
WESTERN
UNION : Receiver Name :- GHALIB NASSOR MONERO.
Tunawashukuru
kwa Michango yenu ya hali na Mali.
Na
mtumishi wenu katika kheri .
GHALIB
NASSOR MONERO L AZHARY .