Kada
wa Chama Cha Mapinduzi Edmund Rutaraka aliyetangaza nia ya kugombea
jimbo la Moshi mjini.
SIKU chache baada ya kumalizika
mchakato wa kumpata kada atakaye
peperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kinyang’anyiro cha
kumpata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Makada wa chama hicho
sasa wamerejea majimboni na kuanza harakati za kuwania nafasi ya kuteuliwa
kugombea Ubunge..
Hali hiyo inajitokeza katika
jimbo la Moshi mjini ,baada ya vijana wa
chama hicho kuonekana kuhamasika huku wakijitokeza kutangaza nia ya kuwania
nafasi ya Ubunge na kutishia harakati za baadhi ya makada wakongwe ndani ya
chama hicho.
Waliojitokeza na kutangaza nia
hadharani hadi sasa ,Mjumbe wa mkutano
mkuu wa CCM na naibu kamanda wa Vijana CCM manispaa ya Moshi ,Edmund
Rutaraka(37) na Mwenezi wa Chama hicho wilaya ya Moshi mjini Priscus
Tarimo,diwani wa kata ya Kilimanjaro aliyemaliza muda
wake.
Rutaraka ambaye ni msomi mwenye
Shahada ya Uzamili,(M.BA) ya Chuo cha Uongozi ,Esami na Shahada ya Sayansi ya Chakula na
teknolojia ya Chuo kikuu cha Sokoine (SUA),alisema CCM katika jimbo la Moshi
mjini kwa sasa kinapaswa kumsimaisha mtu mwenye hekima,Busara na Mcha
Mungu.
“Kiongozi kwa sasa atakaye tosha
kupeperusha chama chetu ni yule atakaye
weza kusimamia vema rasirimali zilizopo katika jimbo letu na si yule mwenye
maneno ya kulaghai wananchi”alisema Rurataka.
Rutaraka ambaye pia ni mjumbe wa
mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi
alisema baada ya kushauriwa na wazee, kujitathmini na kupima uwezo wake
ameona anatosha kuwawakilisha wananchi wa jimbo la Moshi mjini
.
“Nimeshauriwa na
wazee,nikajitathimini na kupima nikaona kwamba
ninatosha kuwa mwakilishi mwema wa wananchi wa jimbo la Moshi mjini .hivyo basi
naomba nitumie muda huu kutangaza rasmi nia ya kugombea ubunge katika jimbo la
Moshi mjini.”alisema Rutaraka ambaye pia ni naibu kamanda wa vijana wa CCM
manispaa ya Moshi.
Alisema kwa namna hali ilivyo
sasa chama Cha Mapinduzi kinapaswa
kuwa na viongozi vijana ambao wataweza kuliongoza taifa kwa ujumla, kwani
vijana ndio wenye nguvu na ambao wanaweza kuleta mabadiliko kwa haraka
zaidi.
Rutaraka alisema kama kijana
ameamua kugombea nafasi ya ubunge katika
jimbo la Moshi mjini ili kulikomboa kutoka Upinzania na kurudi Chama cha
Mapinduzi huku akiwaomba vijana wenzake kumuunga mkono .
“Kazi ya mbunge ni kuisimamia na
kuishauri serikali hivyo basi
uwezi kufanya hivyo kama huna dhamira ya kweli ya kuingia kwenye bunge kwa
ajili ya kufanya kazi ya wananchi.”alisema Rutaraka
Kuhusu vipaumbele vyake Rutaraka
alisema ni kuhakikisha huduma za afya
zinapewa nafasi ya kwanza hasa kwa Mama wajawazito na watoto na kwamba huduma
muhimu hazikosekani katika Hospitali,Zahanati na vituo vya Afya vilivyoko ndani
ya jimbo la Moshi mjini.
Mbali na kipaumbele hicho
Rutaraka pia alisema atahakikisha anawatetea
walemavu wa aina zote ikiwa ni pamoja na kusaidia angalau wanapata nafasi ya
kufanya kazi ambazo wanauwezo nazo.
Pia alisema atahakikisha
anasimamia miundo mbinu na kusaidia watu
wanapata hati za viwanja vyao kwani kuna baadhi ya kata wananchi
wanashida ya ardhi na viwanja havijapimwa katika manispaa.
Kujitokeza kundi hilo la
vijana kunafanya idadi ya makada wa chama
hicho walioonesha nia ya kutaka kugombea Ubunge katika jimbo hilo lililoomgozwa
na Philemoni Ndesamburo (Chadema) kufikia 12 hadi sasa licha ya uwepo wa
baadhi yao kungojea kukamilika kwa mkutano mkuu wa Chama hicho mjini
Dodoma.