Kamanda wa Vijana akikagua timu ya Muembeladu wakati wa mchezo wa mwisho wa
Bonaza la Masauni Cup.linalofanyika uwanja wa malindi Zanzibar, Mchezo huo
umeshindwa kumalizika kutokana na Viongozi wa timu ya Muembeladu kuitoa
timu yao kwa madai ya mchezaji wa timu ya Mkunazini kudaiwa kumpiga mpenzi
wa timu hiyo.
Kamanda wa Vijana akikagua timu ya Mkunazini wakati wa mchezo wa mwisho wa
Bonaza la Masauni Cup.linalofanyika uwanja wa malindi Zanzibar, Mchezo huo
umeshindwa kumalizika kutokana na Viongozi wa timu ya Muembeladu kuitoa
timu yao kwa madai ya mchezaji wa timu ya Mkunazini kudaiwa kumpiga mpenzi
wa timu hiyo.
Kikosi cha timu ya Muembeladu kilicho shindwa kumaliza mchezo wao wa mwisho
na timu ya Mkunazini timu hii ilihitaji ushindi wa mabao 3--0 ili kuweza
kusonga mbele ya Bonaza hilo kuingia nusu fainali, mchezo huo umemalizi
kabla ya wakati wake zikiwa zimebaki dakika 4 mchezo kumalizika.
Kikosi cha timu ya Mkunazini kinachotinga Nusu Fainali leo usiku katika
viwanja vya Mnazi mmoja na Timu ya Kikwajuni Juu.
Kocha wa timu ya Muembeladu akitowa maelezo kwa wachezaji wa timu yao kabla
ya kuaza kwa mchezo wa Bonaza Masauni Cup.
Wachezaji wa Timu ya Mkunazin wakiwania mpira wakati wa mchezo huo wa
mwisho kukamilisha mzunguko wa kwanza.
Kipa wa timu ya Mkunazini akiokoa mpira
wakati wa mchezo wao na timu ya Muembeladu
Mchezaji wa timu ya Mkunazini
akimpita mchezaji wa timu ya Muembeladu.
Mchezaji wa timu ya Muembeladu akiwa na mpira baada ya kumpita mchezaji wa
timu ya Mkunazini akiwa chini.
Kiongozi wa Timu ya Mkunazini akitowa maelezo kwa wachezaji wake wakati wa
mapumziko ya kipindi cha kwanza timu hizo zikiwa sare bila ya
kufungana.
Golikipa wa timu ya Mkunazini akitowa maelezo kwa wachezaji
wake.
Kocha Timu ya Muembeladu akitowa maelezo ya ushindi kwa wachezaji wake
wakati wa mapumziko,Timu ya Muembeladu ilihitaji kushinda 3--0 ili kuweza
kuingia nusu fainali yo Bonaza hilo.
Mchezaji wa timu ya Mkunazini akiokoa mpira golini kwake huku mchezaji wa
timu ya Muembeladu akiwa karibu
Mchezaji wa timu ya Mkunazini akimpita mchezaji wa timu ya Muembeladu
wakati wa mchezo wao wa mwisho wa Bonaza Masauni Cup.Timu hizo zimetoka
sare, baada ya mchezo huo kuvunjika kutokana na fujo za wapenzi wa timu
hiyo
Mchezaji wa timu ya Mkunazini anayedaiwa kampiga gunu mpenzi wa timu ya
Muembeladu wakati akiokoa mpira na kuagukia katika eneo la timu hiyo na
kutokea fujo hiyo iliosababisha mchezo huo kuvunjika zikiwa zimebaki dakika
nne za mchezo huo.
Kiongozi wa Timu ya Mkunazini na Mchezaji wa Zamani wa timu ya Taifa Amour
Azizi akimsihi kocha wa timu ya Muembeladu kuendelea na mchezo huo baada ya
kuchukua uamuzi wa kuitoa timu yake nje
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia