Katibu wa baraza la wazazi wa chama cha mapinduzi ccm mayasa kimbau wa pili kutoka kushoto (picha na maktaba) |
Katibu wa
baraza la wazazi wa chama cha mapinduzi ccm mayasa kimbau amewataka wanaccm
kuunganisha nguvu pamoja na kuacha makundi kwa kuwa tayari chama hicho
kimemshampata mgombea uraisi ambaye Ni John Pombe Magufuli.
Kimbau aliyasema
hayo jana katika kata ya kaloleni wakati akiwanadi wagombea ubunge wa chama cha
mapinduzi ccm ambao wapo katika ziara ya kuzunguka katika kata zote za jimbo la
arusha mjini ili kunadi sera zao.
Alisema kuwa
wapo wanaccm ambao bado hawajavunja makundi kwa kuwa huenda mgombea waliyemtaka
hajapitishwa ambapo alisema kuwa chama hicho ni imara katika kufanya uteuzi kwa
mgombea nayekubalika.
“Ccm wote
sasa ni wamoja tuelekeze Nguvu zetu zote katika kuhakikisha kuwa ccm inacghukua
dola na tayari tunae John Pombe Magufuli ambaye anatosha kupeperusha bendera ya
chama cha mapinduzi hivyo basi kwa sasa kazi yetu ni kutafuta kura tu nasi
vinginevyo”alisema Kimbau
Katika hatua
nyingine kimbau alisema kuwa enzi za chama kubeba watu mizigo zimepita na
kuwataka wagombea wote kunsadi sera zao na kufuata taratibu kwa kuwa swala la
rushwa halina nafasi kwa sasa.
Alisema
wanachoangalia kwa sasa ni kuhakikisha kuwa chama kinapitisha mgombea ambaye
anakubalika na wananchi na sio chama ili kuhakikisha kuwa jimbo la Arusha mjini
linarudi mikononi mwa ccm.