katika picha ni mwanadada
Phidesia Mwakilima
Phidesia Mwakilima
Na Woinde Shizza,wa libeneke la kaskazini blog
Mkurgenzi wa kampuni ya Phide Intataiment ambaye pia ni meneja masoko wa kituo cha redio Triple A ya Arusha, Phidesia
Mwakilima, ameibuka kidedea kwenye uchaguzi wa mbunge viti maaluimu kupitia
jumuia ya wazazi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha.
Phidesia Mwakilima, amepata kura 18 na kuwashinda, Aimbora
Nnko, aliyepata kura 6, Angela Mwanri kura 4 na Anna John kura 2 ,uchaguzi huo
umefanyika ukumbi wa ccm, mkoa.
Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo katibu wa jumuia ya
wazazi mkoa, wa Arusha, Mayasa Kimbau, amewataka wale ambao kura zaohazikutosha
kutokukata tamaa bali wajipange kwa chaguzi zingine ndani ya chama.
Akawataka wanawake wasiwe wanyonge kujitokeza kugombea
nafasi mbalimbali za uongozi bali wawe mstari wa mbele kujitokeza kila uchaguzi
utakapotokea