Picha ya
Post iliyopostiwa na Kijana ajulikanae kama Raffayel
Mombury.
Kampuni
ya Proin Promotions Ltd ambao ni waandaaji na waendeshaji wa shindano la
Kusaka vipaji vya Kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT)
ambalo linaendelea kufanyika huku washiriki watano Wakiwa washaenguliwa
katika shindano hilo Kutokana na Kutokupata kura za kutosha kutoka kwa
watazamaji wa Kipindi hiko mahiri kinachorushwa na kituo cha runinga cha
ITV siku ya jumapili saa tatu na nusu usiku.
Proin
Promotions tunasikitika kusema kuwa kuna habari ambazo sio za kweli ambazo
zimepostiwa katika ukurasa wa facebook wa kijana mmoja ajulikanae kwa jina
la Raffayel
Mombury ambae amepost taarifa hiyo yenye kichwa cha Habari
"WASHIRIKI WA TMT 2015 WAFUMANIWA
WAKINGONOKA" kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu, Sisi kama
Proin Promotions ltd tunapenda kusema kuwa taarifa hizo hazina ukweli
wowote na sura hizo hatuzitambui na wala sura zinazoonekana katika post
hiyo sio za washiriki wetu wa TMT 2015 na hazijawahi
kuwa.
Kutokana
na post hiyo ambayo yenye mlengo wa kuichafua Kampuni ya Proin Promotions
Ltd ambao ndio waandaaji na waendeshaji wa shindano pamoja na mradi mzima
wa TMT ambao unaaminika Tanzania Nzima na Nje ya Tanzania tumepata usumbufu
mwingi kutoka kwa wapenzi wa Shindano hilo pamoja na wazazi wa Washiriki
waliobakia. Tunapenda kusema kuwa kiukweli taarifa hizo zimetuletea
usumbufu mkubwa sana na kupelekea kuvunja imani kwa watazamaji wetu na
wapenzi wa vipindi vyetu, Sisi kama Proin Promotions tunawaomba Watanzania
na Wapenzi wa TMT kuzipuuza taarifa hizo na hakuna kitu kama hiko
kwasababu Nyumba wanayoishi washiriki wa TMT 2015 imezingatia maadili
makubwa na kuwepo kwa usimamizi wa matron katika kambi
hiyo.
Proin
promotions tunasema kutokana na taarifa hizi kutokuwa na ukweli wowote
tunaahidi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu huyu aliyesambaza taarifa
hizi za uongo na zilizotuletea usumbufu mkubwa sana katika jamii
inayofuatilia shindano hili na kupelekea kupoteza imani kwa
jamii.
Imetolewa
na
Idara ya
Mahusiano ya Umma
Proin
Promotions Ltd