BREAKING NEWS

Thursday, July 2, 2015

POLISI ARUSHA KUWAFANYIA USAILI ASKARI WATARAJIWA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Liberatus Sabas 
Na woinde shizza,arusha

Jeshi la Polisi Mkoani hapa linatarajia kuwafanyia usaili vijana wa Mkoa huu waliomaliza kidato cha nne mwaka 2014 ambao wamechaguliwa kupitia tovuti ya Tamisemi ambayo ni www.pmoralg.go.tz.  Wanaotarajia  kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Liberatus Sabas aliyasema hayo ofisini kwake leo asubuhi ambapo alisema zoezi hilo litafanyika kwa muda wa siku mbili mfululizo yaani kuanzia tarehe 06.07.2015 na tarehe 07.07.2015 katika ofisi za Makao Makuu ya Polisi za Mkoa huu.

Aidha alisema zoezi hilo litaanza kuanzia saa 02:00 Asubuhi hadi saa 10:00 Jioni huku tayari majina ya vijana waliochaguliwa na maelezo yake yameshabandikwa katika ofisi za Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Mkuu wa wilaya ya Arusha na Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa wilaya ya Arusha Mjini huku wilaya za Longido, Arumeru, Monduli, Karatu na Ngorongoro majina yao yatabandikwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri husika za wilaya hizo.

Waombaji watatakiwa wawe na vyeti vyote vya masomo (Academic Certificate(s)/Result Slip(s) & Leaving Certificate(s) na nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (original Birth Certificate) huku Hati ya Kiapo cha kuzaliwa haitakubaliwa pia atatakiwa kuwa na namba za simu ambayo itasaidia kumjulisha endapo atachaguliwa.

Aidha Kamanda Sabas alisema kwamba kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili huku atatakiwa kuwa na kalamu ya wino kwa ajili ya usaili wa kuandika bila kusahau kuzingatia tarehe na muda kuanza usaili.

Kamanda alimalizia kwa kusema kwamba, Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye ili mradi awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates