Wanafunzi wa Skuli ya msingi Rahale wakimpokea Waziri wa Uwezeshaji Ustawi
wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab Omar alipowasili katika
viwanja vya Skuli hiyo kukabidhi Vifaa viliotolewa na Mwakilishi wa Rahaleo
kwa Wananchi wa jimbo hilo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe. Zainab
Omar akiwasili katika viwanja vya Skuli ya Msingi Rahaleo kuhudhuria hafla
ya kukabidhi Vifaa kulia Mwakilishi wa Rahaleo na kushoto Mwenyekiti wa
Kamati ya Skuli ya Rahaleo Ndg Daudi Amani Bakari
Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira akizungumza wakati
wa hafla ya kukabidhi Vifaa kwa Wananchi wa Jimbo lake iliofanyika katika
Skuli ya Msingi Rahaleo Zanzibar.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe. Zainab
Omar, akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Rahaleo na wanafunzi wa skuli
hiyo katika hafla ya kukabidhi vifaa vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo
hilo Mhe. Nassor Salim Jazira.
Wanafunzi wa skuli ya msingi rahaleo wakimsikiliza Mhe Waziri Zainab
akitowa nasaha zake wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa
Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Rahaleo wakifuatilia nasaha za Mhe Waziri
Zainab wakati akizungumza na Wananchi wa jimbo la Rahaleo katika hafla ya
kukabidhi vifaa,
Wazee wa Kamati ya Jimbo la Rahaleo
wakimsikiliza Waziri Zainab Omar akiwahutubia.
Walimu wa Skuli ya Rahaleo wakifuatilia hafla hiyo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab
Omar akimkabidhi Seti ya Komputer
Mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu Rahaleo,kwa ajili ya matumizi ya Chuo hicho
vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira,
hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Skuli ya Rahaleo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii
Vijana Wanawake na Watoto Mhe. Zainab Omar, akimkabidhi Seti ya Vifaa vya
ufundi gereji Kijana Zuberi Issa Ford,kwa ajili ya matumizi ya kazi zao za
ufundi wa pikipiki vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo
Mhe Nassor Salim Jazira, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Skuli
ya Rahaleo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii
Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab Omar, akimkabidhi Vyerehani Mkuu wa Kituo cha Elimu
Mbadala Rahaleo Zanzibar Bi Hawa Seif Amour, kwa ajili ya matumizi ya
Wanafunzi wa Kituo hicho,vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo
Mhe Nassor Salim Jazira, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Skuli
ya Rahaleo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii
Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab Omar akimkabidhi Seti ya Komputer Mkuu
wa Chuo cha Ualimu Rahaleo Ndg Ussi Said Suleiman, kwa ajili ya matumizi ya
Chuo hicho vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim
Jazira, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Skuli ya
Rahaleo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab
Omar akimkabidhi fedha Mkuu wa Chuo cha Ualimu Rahaleo Ndg Ussi Said
Suleiman, kwa ajili ya kuogezea kusajili Chuo chao NACTE,fedha hizo ikiwa
ahadi alioyowaahidi Viongozi wa Chuo hicho kwa ajili ya kufanya usajili wa
Taifa.
Mzee wa kamati ya Jimbo la Rahaleo Ali
Vuai Mussa akisoma dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya kukabidhi
vifaa kwa wananchi wa jimbo la rahaleo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii
Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Zaiba Omar, na Mwakilishi wa Jimbo
la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi
wa Kamati ya Jimbo la Rahaleo, baada ya hafla hiyo ya kukabidhi vifaa.
ilofanyika katika skuli ya rahaleo Zanzibar.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe
Zaiba Omar, na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira
wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Rahaleo,
baada ya hafla hiyo ya kukabidhi vifaa. ilofanyika katika skuli ya rahaleo
Zanzibar.