LG YATOA PUNGUZO KABAMBE LA BEI YA BIDHAA ZAKE KIPINDI HIKI CHA RAMADHANI NA SABASABA

IMG_5470
Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya MeTL Group, Bi. Fatema Dewji-Jaffer akipokea taarifa ya shughuli mbalimbali zinazoendelea kwenye maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba” kwa mmoja wa maafisa wa kampuni ya bidhaa za LG Tanzania ambapo kampuni ya Mohammed Enterprises Limited Tanzania (MeTL) ndio msambazaji rasmi wa bidhaa hiyo nchini kabla ya hafla fupi ya uzinduzi wa friji mpya ya LG yenye milango pacha aina ya “Velvet Gardenia na Coral Irish”.
2
Mmoja wa wakurugenzi wa LG toka Korea, Bw. Billy Kim (Kulia) akizindua rasmi friji mpya ya LG yenye milango pacha aina ya “Velvet Gardenia na Coral Irish” katika banda la LG ndani ya viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba” anayeshuhudia (kushoto) ni Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya MeTL Group ambao ni mawakala pekee wa usambazaji wa bidhaa za kampuni ya LG, Fatema Dewji-Jaffer.
IMG_5552
Mkufunzi mwandamizi toka kampuni ya LG Tanzania, Bi. Elizabeth Morris (katikati) akifafanua zaidi kwa waandishi wa habari hawapo pichani aina mpya ya friji ya LG yenye milango pacha aina ya “Velvet Gardenia na Coral Irish” wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo mpya, katika viwanja vya maonyesho ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”. Kulia ni Mkurugenzi wa LG, Mohan Kumar na mmoja wa wakurugenzi wakuu wa LG toka Korea Bw. Billy Kim pamoja na Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya MeTL Group ambao ni mawakala pekee wa usambazaji wa bidhaa za kampuni ya LG, Fatema Dewji-Jaffer (wa pili kushoto).

Kampuni ya LG Tanzania imetangaza ofa kabambe ya punguzo la bei za bidhaa zake, itakayodumu katika kipindi chote cha maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba ikiwa ni kuadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Meneja mwandamizi wa LG, Bw. Kim Taehoon amesema wateja watakaonunua bidhaa za LG katika kipindi hiki cha Ramadhani na Sabasaba watafurahia punguzo la bei la hadi asilimia 15, pamoja na ofa nyingine za kuvutia zikiwemo zawadi za bure.
Bw. Kim pia ametumia fursa hiyo kuitambulisha friji mpya za LG yenye milango pacha aina ya “Velvet Gardenia” na “Coral Irish” kwa mara ya kwanza kabisa katika soko la Tanzania na kuthibitisha kuwa kampuni ya Mohammed Enterprises Limited Tanzania (MeTL) kuwa msambazaji rasmi wa bidhaa hiyo nchini.
Amesema friji hizo zina nafasi kubwa na nyingi za kuhifadhia vyakula, uwezo wa kuzuia bakteria na hivyo kutunza vyakula katika hali ya usalama wa kiafya.
Friji hizo zina makabati yaliyojengewa kwa ndani katika milango yake, ambapo aina hiyo ya milango huja pamoja na kioo imara.
Amesema friji hizo zinatumia teknolojia mpya ya LG “Smart Inverter Compressor” ambayo ina uwezo wa kupunguza matumizi ya umeme hadi asilimia 36.
Bw. Kim amewashauri watanzania kuchangamkia fursa ya bidhaa hizo mpya zilizoingia sokoni na kuwahakikishia kuwa watastaajabishwa na ubora na uwezo wa friji hizo,
Amesema kuwa Friji hizo pia zitapatikana katika maduka mengine yote yanayouza vifaa vya kielektroniki jijini Dar es Salaam.
Ameongeza kuwa katika kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa Ramadhani, watu wengi hutunza vyakula vyao kwenye friji na ni hulka ya wengi kuamka usiku kwa ajili ya kupata Daku, hivyo bidhaa hii itakuwa na manufaa sana kwao, kwani ina uwezo wakulinda dhidi ya unyevunyevu na pia kutunza chakula katika hali ya usalama.
Ofa hizi zitadumu kipindi chote za mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja na Sabasaba, hii ni katika kuwapa wateja wa LG muda wa kutosha kujipatia bidhaa za LG zenye punguzo la bei
Bw. Kim Taehoon amesisitiza kuwa kampuni ya LG Electronics daima inaendelea kuboresha mfumo wa teknolojia ili kuleta bidhaa zenye ubora na muonekano yakinifu, ili kufikia viwango vya matumizi ya kimataifa.
Amesema toka kuanzishwa kwake mwaka 1958, LG inaendelea kuzalisha bidhaa zinazoendana na mahitaji ya wateja wake na uingizwaji wa bidhaa hii mpya sokoni ni muendelezo wa matoleo ya teknolojia, ambayo yanatengenezwa na kuboreshwa kulingana na matakwa na mahitaji ya wateja.
IMG_5580
5
Mkufunzi mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris, (kushoto) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) ubora wa kompresa za friji za kampuni ya LG ambazo ni imara na zinahimili hali ya hewa ya mazingira yoyote wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo mpya katika viwanja vya maonyesho vya sabasaba.
IMG_5657
Mkufunzi mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris, (kushoto) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) bidhaa nyingine za LG ambazo zipo kwenye ofa ya punguzo la bei la asilimia 15 katika msimu huu wa sabasaba na Ramadhani ndani ya banda la MeTL Group.
IMG_5663
Waandishi wa habari wakiangali moja ubora wa TV za LG kwa kutumia miwani ya 3D inapoivaa inakuonyesha uhalisia wa picha unayoitaza kwa ukaribu zaidi wakati uzinduzi wa moja ya bidhaa za LG katika banda la kampuni ya MeTL Group kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam.
IMG_5610
Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya MeTL Group ambao ni mawakala pekee wa usambazaji wa bidhaa za kampuni ya LG, Fatema Dewji-Jaffer akimkabidhi zawadi kutoka MeTL, Mkurugenzi wa kampuni ya LG toka Korea, Bw. Billy Kim mara baada ya uzinduzi huo katika banda la MeTL Group.
IMG_5618
Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya MeTL Group ambao ni mawakala pekee wa usambazaji wa bidhaa za kampuni ya LG, Fatema Dewji-Jaffer akiendelea na zoezi la kukabidhi zawadi kwa maafisa wa kampuni ya LG Tanzania.
IMG_5647
Meneja wa LG tawi la Nkurumah, Bw. Yasin Lodhi akizungumza na waandishi wa habari ambapo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha watanzania kutembelea banda la LG na kununua bidhaa mbalimbali zenye ubora wa hali juu na zipo katika punguzo la bei la asilimia 15 ya kila bidhaa katika kipindi hichi cha sabasaba na mwezi huu wa Ramadhani.
IMG_5620
Mkufunzi mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi huo. Wa tatu kulia ni Meneja wa LG tawi la Nkurumah, Bw. Yasin Lodhi.
IMG_5468
Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya LG Tanzania na MeTL Group wanaotoa huduma kwenye cha maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kutimua vumbi viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post