UONGOZI MPYA AICC SQUASH KLABU KUANDAA MASHINDANO YA NDANI.



  Baada ya kufanikiwa kupata uongozi mpya ,klabu ya AICC Squash imejipanga
kuandaa mashindano ya mchezo huo yakayoshirikisha wachezaji mbalimbali.


Mikakati hiyo Imekuja mweza mmoja baada ya klabu hiyo kupata uongozi mpya
ambao utaongoza kwa muda wa mwaka mmoja hadi juni mwakani.


Viongozi waliochaguliwa ni Mwenyekiti  Adolf Olomi,Makamo mwenyekiti
Innocent Mapendo,Katibu  mkuu Emily Shayo,katibu Masidizi Emmanuel Mtei,
pamoja na mweka hazina  Moses Ephraim.



Katibu mkuu wa AICC Squash klabu Emily Shayo alieleza kuwa  wao kama
viongozi wapya watahakikisha mchezo wa squash unakuwa na kuendelea ili
kuweza kuifanya klabu hiyo na mkoa wa Arusha unakuwa na wachezaji wenye
uwezo tofauti na miaka ya nyuma.


“Tumejipanga kwa mwaka huu kuweza kuwa na mashindano yetu ya ndani
ambayo  yatawashirrikisha
wachezaji waliopo ndani ya klabu na baadhi ya vilabu vilivyo ndani ya
Arusha ili kuweza kuwaweka sawa wachezaji wetu katika kujiandaa na
mashindano mbalimbali ya ndani na nje.”alisema Shayo.


AICC Squash klabu ina jumla ya washiriki 30 ambao wakubaliana katika
kuhakikisha chama kinakua na mikakati ambayo itakiwezesha chama kujiendesha
ambapo kila mshiriki atalipia sh. Elfu kumi na tano 15,000/= kwa mwezi .
aliongeza.





“Pia tunataraji kabla ya mwisho wa mwaka tutaandaa mashindano makubwa
ambayo tutaalika vilabu kutoka Dar es salaam na Zanzibar li kuweza
kukutanisha wachezaji hao ambao itawafanya kuweza kuwaongeza ushindani kwa
kujipatia ujuzi mpya”Alisema Shayo.



Aidha AICC Squash inasisitiza vijana  wajitokeze  katika kuucheza mchezo
huu ambao utawawezesha kunyanyua na kukuza vipaji vyao.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post