Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar Ndg Adila
Hilal Vuai, akiutambulisha Ujumbe wa Madaktari Diaspora kutoka Washington
walioletwa na Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Washington wakali
walipofika katika Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar walipofika hapo kutowa
Elimu ya Afya ya Saratani ya Matiti na Mano, wakiwa Zanzibar kwa uwenyeji
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora na Benki ya Watu wa Zanzibar
(PBZ)
Rais wa Jumuiya ya Watanzania Washinton Ndg Iddi Sandaly akiutambulisha
Ujumbe wa Madaktari 17 Diaspora, waliofika Zanzibar kutoa Tiba ya Maradhi
ya Saratani ya Matiti, Kisukari na Meno akitowa maelezo wakati walipofika
katik Chuo cha Elimu ya Afya Mombasa Zanzibar, na kutowa Elimu ya kutambua
Saratani ya Matiti kwa Kinamama. na kutowa huduma ya uchunguzi wa
Meno.
Rais wa Jumuiya ya Wanawake Afrika Washington (Africa Womens Cancer
Awereness Association ) Dr Ify Anne Nwabukwu, akiutambulisha ujumbe wa
Madaktari wa maradhi mbalimbali waliowasili Zanzibar kwa ajili ya kutowa
huduma kwa wananchi wa Zanzibar ikiwa ni kusaidia Wafrika wenzao walioko
Afrika.
Rais wa Jumuiya ya Wanawake Afrika Washington (Africa Womens Cancer Awereness Association ) Dr Ify Anne Nwabukwu, akiutambulisha ujumbe wa Madaktari wa maradhi mbalimbali waliowasili Zanzibar kwa ajili ya kutowa huduma kwa wananchi wa Zanzibar ikiwa ni kusaidia Wafrika wenzao walioko Afrika.
Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar wakimsikiliza Dr Ify akitowa
maelezo na kuwatambulisha Madaktari Diaspora aliofuatana nao.
Dr Ify Anne Nwabukwu akitowa Elimu ya tambua viashiria vya Saratani ya
Matiti kwa wanafunzi hao wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar,
Dr Ify akitowa mada kuhusiana na Saratani ya Matiti kwa Wanafunzi wa Chuo
hicho hutoa Elimu ya Udaktari wa aima mbalimbali chuoni hapo.
Dr Ify akionesha Mashine ya kupimia Saratani ya Matiti ya Kisasa inayoitwa
MamaGram hutumika kucunguza viashiria vya Saratani ya Matiti kwa Wanachuo
hao wakati akitowa Elimu ya Saratani ya Matiti jinsi ya kumgundua Mwanamke
mwenye matatizo hayo.
Wanafunzi wa Chuo hicho
wamepata fursa ya kuuliza mswali wakati wa Mafunzo hayo.
Mmoja wa Madaktari hayo akitowa mfano hai kutokana na matatizo ya Saratani
ya Matiti, kwa Wanachuo hao.
Daktari wa Meno Bi Queenate Ibeto akitowa elimu ya kutunza meno na kinga ya
mane kwa Wanafunzi hao jinsi ya kuyatunza meno. wakati walipofika Chuoni
hapo kutowa Elimu kwa Wanachuo hicho.
Daktari wa Meno Venessal Quitero akionesha moja ya tiba ya kunusuru meno
kwa wanafunzi hao wakati wakitowa Elimu ya Utunzaji wa Meno na tiba
yake.
Mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar akionesha mafunzo ya utunzaji
wa Meno kwa vitendo jinsi ya kupiga msuwaki inavyotakiwa kuweza kuimarisha
meno kuwa imara
Dr Queenate Ibeto akionesha mfano ya vitendo kwa mmoja wa mnafunzi wa Chuo
hichi jinsi ya utumiaji wa msuaki katika kupiga kwa Wanafunzi hao, wakati
walipofika kutoa Elimu ya Afya kwa Wanafunzi wa Chuo hicho Mombasa
Zanzibar.
Profesa Hailu na Dr Quintero wakifuatilia Mada zilizokuwa zikiwakilishwa
kuhusiana na Saratani ya Matiti na Tiba ya Meno, kwa Wanafunzi wa Chuo cha
Elimu ya Afya Zanzibar Mombasa wakati walipofika katika Chuo hicho wakiwa
Zanzibar kwa ajili ya kutoa Tiba ya Saratani ya Matiti Ugonjwa wa Kisukari
na Meno.
Dr Quintero ni mtaalamu ya Magonjwa ya Meno akifafanua moja ya swali
lililoulizwa na Wanafunzi wa Chuo hicho.
Mwanafunzi wa chuo hicho akiuliza swali kuhusiana na baadhi ya Wananchi
meno yao huwa na ukungu mweusi kwa wataalam hao
Madaktari wa Diaspora wakigawa misuwaki na dawa za meno kwa wanafunzi hao
baada ya kutowa Elimu chuoni hapo,
Dr Silvia Dasi akitowa maelezo kwa
wanafunzi hau jinsi ya kumgundua mwanamke mwenye matatiti ya Saratani ya
Matiti wakati wakifanya mafunzo hayo kwa wanafunzi hao wanaochukua Elimu ya
Afya ya binadamu,
Dr Silvia Dasi akitowa maelezo kwa wanafunzi hau jinsi ya kumgundua
mwanamke mwenye matatiti ya Saratani ya Matiti wakati wakifanya mafunzo
hayo kwa wanafunzi hao wanaochukua Elimu ya Afya ya binadamu,
Dr Ify akitowa Elimu ya Vitendo
kugundua viashiria vya Saratani ya Matiti kwa Mwanamke akitowa mafunzo hayo
ya mmoja wa mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar.
Dr Ify akitowa Elimu ya Vitendo kugundua viashiria vya Saratani ya Matiti
kwa Mwanamke akitowa mafunzo hayo ya mmoja wa mwanafunzi wa Chuo cha Elimu
ya Afya Zanzibar kulia Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora
Zanzibar Ndg Adila Hilal Vuai,
Madaktari Diaspora wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Wanafunzi wa Chuo
cha Elimu ya Afya Zanzibar baada ya kutoa Elimu kwao,
DR Queenate Ibote akimfanyia uchunguzi wa meno mmoja wa wanafunzi wa Chuo
cha Elimu ya Afya Zanzibar wakati walipofika Chuoni hapo kutowa Elimu kwa
Wanachuo hicho.
DR Queenate Ibote akimfanyia uchunguzi wa meno mmoja wa wanafunzi wa Chuo
cha Elimu ya Afya Zanzibar wakati walipofika Chuoni hapo kutowa Elimu kwa
Wanachuo hicho.
DR Queenate Ibote akimfanyia uchunguzi wa meno mmoja wa wanafunzi wa Chuo
cha Elimu ya Afya Zanzibar wakati walipofika Chuoni hapo kutowa Elimu kwa
Wanachuo hicho.
Madaktari wa Diaspora wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Chuo
cha Elimu ya Afya Zanzibar wakiwa nje ya jengo la Chuo hicho katika Skuli
ya Sekondari ya SHAA Mombasa Zanzibar.
Picha na OthmanMapara.Blog Zanzinews.Com
Picha na OthmanMapara.Blog Zanzinews.Com