Mbunge
wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akizungumza katika uchaguzi wa
kumpata Mbunge pamoja na Mbunge viti maalum kupitia chama cha Demokrasia
na maendeleo(CHADEMA)jijini Arusha ambapo aliibuka kidedea kwa kura 255
sawa na asilimia 93.06% (Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Mbunge
viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Joyce
John Mukya alipata kura 39 sawa na asilimia 73.6% katika kinyang'anyiro
hicho hivyo kumfanya kuwa Mbunge wa viti maalum,aliwataka wajumbe wa
mkutano huo kuvunja makundi ili kuhakikisha chama kinashinda katika
uchaguzi wa Urais,Ubunge na udiwani
Mgombea
kupitia chama cha Demokrasia na maendelao (CHADEMA)Noel Olevaroya
akizungumza mara baada ya kutangazwa kushika nafasi ya pili kwa kupata
kura 13 sawa na asilimia 4.74% katika kinyang"anyiro hicho ambapo
aliwashukuru wajumbe wa mkutano huo na kuhaidi kumpa Mbunge Lema
shilingi laki tano kwaajili ya kampeni ya kuhakikisha chama hicho
kinapata ushindi wa kishindo
Wagombea ubunge viti maalum Mkoa wa Arusha wakisubiria kuingia kujinadi kwa wajumbe wa mkutano
Mgombea
nafasi ya Ubunge,Nsajigwa Mwakatobe aliyepata kura 6 sawa asilimia
2.18% akiwashukuru wajumbe wa mkutano pamoja na wanachama wa chama hicho
PIPOOOOZ!Mgombea
nafasi ya Ubunge viti maalum Grace Macha katika
kinyang'anyiro hicho , akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo na kuhaidi
kushirikiana nao
Mgombea nafasi ya Ubunge viti maalum Glory Bernad akishukuru katika mkutano huo
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akisaini fomu ya uchaguzi,pembeni ni Mbunge wa Rombo na mwenyekiti wa uchaguzi huo Joseph Selasini
Mbunge wa Rombo na mwenyekiti wa uchaguzi huo Joseph Selasini akitaja washindi katka kinyang'anyiro hicho
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa na mtoto wake aliyemkimbilia mara baada ya baba yake kutangazwa mshindi katika uchaguzi huo
Wajumbe wakimshangilia Mbunge viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Joyce John Mukya
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia