Na Woinde Shizza,libeneke la kaskazini blog
Mwendesha magari Randeep Shingh kutoka
jijini Dar es Salam ameibuka mshindi katika mashindano ya kila mwaka ya
mbio za nyika za magari nane-nane rally yaliyotimua vumbi katika
mji wa Arusha mwishoni mwa wiki.
Mashindano hayo yamefanykia kwa siku
mbili mfululizo huku yakishuhudiwa ushindani mkali kwa madereva hao waliotoka
mikoa mbalimbali na Randeep Shingh akiwa na msoma ramani guvinder singh wa gari
ya mistubish lancer akiibuka mshindi wa jumla katika mashindano hayo.
katika mashindano hayo yaliyokuwa
yakitofauti mwaka huu, baada ya kufungiwa mitambo ya kisasa ya kidigitali kwa
kila gari ili kuwezesha ufuatiliwaji wa kila gari na njia zitakazopitia kwa ajili
ya kuhakikisha kuwa hakuna zengwe wala suala la madereva kuiba njia na
hata kupotea porini.
zaidi ya madereva 20 kutoka ndani
na nje ya nchi walioshindana zaidi ya Km 198 huku mshindi wa pili
akiwa ni Raj Pal Dhani na msoma raman Sinder Sudle wakiwana na
ghari la subaru impreza nafasi ya tatu ikiwa imeshikwa na Gurjit Singh .
huku dereva mkongwe wa nchini
tanzania Gerald Miller akiambulia nafasi ya sita, HUKU baadhi ya madereva
walioshiriki katika mashindano hayo wakisema yalikuwa magumu mwaka huu huku
wengine wakizungumzia changamoto ya barabara
baadhi ya mashabiki wa mchezo
waliojitokeza kwa wingi kutazama mashindano ya hayo ya utrack nanenane
rally walisema wamefurahi na kuiomba serikali kuwezesha mashindano haya
kufanyika mara kwa mara