PANJU AWATAKA WANANCHI KUTOKUNUNULIWA KWA SHILINGI ELFU KUMI

SAM_3941Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ya ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM akinadi sera zake mbele ya wanachama  jijini Arusha ili kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea wa ubunge jimbo la Arusha kupitia CCM.
SAM_4058Mgombea Ubunge ambaye pia ni mwandishi wa habari Swalehe Kiluvia wakati akijinadi mbele ya wana CCM jijini Ausha




Mgombea ubunge kupita chama cha mapinduzi CCM Mustafa Panju ambaye pia ni mkurugenzi wa Bushback Safaris amewataka wananchi kuto uza kura zao kwa shilingi elfu kumi kwa kiongozi yeyote katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu Aliyasema hayo jana wakati akijinadi kwa wananchi na wananchama wa chama hicho, kata ya Baraa jijini Arusha uliohudhuriwa na watiani ubunge 12 jimbo la Arusha mjini Panju alisema kuwa wana CCM wanatakiwa kuchagua kiongozi sahihi ambaye ataleta maendeleo kwa wanachama na wananchi kwa ujumla huku akionya kuwa lazima wanachama wa chama hicho waendeleze sera ya chama ambayo ni kudumisha amani ,upendo na mshikamano kwa Watanzania wote. “Lazima tuwe wamoja, sisi ndio tunakiharibia chama na kusababisha makundi yanayoleta migawanyiko. Tuchague kiongozi mzuri ambaye ataleta maendeleo, pia tuache tabia ya kuuza kura zetu kwa bei ya shilingi 10,000, bora hata uuze kwa laki tano ili ununue walau godoro utakaa nalo kwa miaka mingi” Alisisitiza kuwa chama hicho kitaimarika iwapo tu wanachama na viongozi watashirikiana na kuwa wamoja huku akidai kuwa katika hali ya migawanyiko chama kinaweza kufikia mahali pabaya. Mgombea mwingine katika kinyang’anyiro hicho ambaye pia ni mwandishi wa habari Swalehe Kiluvia wakati akijinadi mbele ya wana CCM katika Kata za Levolosi, Baraa na Kimandolu alisema kuwa endapo atapata ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho atatumia uwezo wake wote aliojaaliwa na Mungu ili kubadilisha hali ya maisha ya wananchi na wapiga kura wa Arusha. Alisema kuwa atakuwa mstari wa mbele kupiga vita rushwa ,uzembe na upotevu wa mali za umma hali itakayosaidia wananchi kupata hak yao.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post