KABLA YA KAMATI KUU CCM KUPIGA PANGA MAJINA YA WAGOMBEA, UVCCM NYAMAGANA WAMWAGA UGALI WA LOWASSA.


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Hussein. A. Kimu amemshutumu waziwazi bila kigugumizi mtangaza nia Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kwa kumhusisha na mipango ya kuaandaa kundi la Mabaunsa na Machinga wa mkoa wa Mwanza kwa lengo la kwenda mjini Dodoma, kushinikiza viongozi wa chama hicho kumchagua mgombea wao na kundi jingine la vijana na akina mama wa CCM kusimama njiani kusimamisha misafara ya wajumbe wa NEC, na Mkutano mkuu wa Chama Taifa kuwapa shinikizo na vitisho wakiwalazimisha warudi na jina la mgombea wao ndugu Edward Lowassa.

Mwenyekiti huyo wa vijana wilaya ya Mwanza mjini (Nyamagana) ameongeza na kudai kuwa yote hayo yalipagwa kufanyika kwa malipo, na kila kijana aliwekewa ahadi ya kulipwa Tsh 100,000/= kwa kila siku, kwa siku zote mpaka mpango ukamilike ... BOFYA PLAY KUSIKILIZA
YAH.TAMKO LA KUPONGEZA KAULI YA MKUU WA MKOA WA MWANZA NDUGU STANSLAUS MAGESA MULONGO.
Ndugu wanahabari na watanzania wote. Kwanza nitumie fursa hii kuwashukuru kwa kuitikia wito na kukubari kuja kuungana nasi kwa lengo la kuwajuza watanzania kwa kile kinachoendelea katika mkoa wetu Wa mwanza kwa faida na manufaa ya watanzania wote.
Siku ya 6/7/2015, mkuu wetu wa mkoa Wa mwanza alitoa maelekezo kwa makamanda wa polisi kuzuia watu wasio kua na malengo mazuri kwa nchi yetu na taifa letu. Wanao kwenda Dodoma kwa lengo la uvunjifu wa amani,katika kipindi hiki cha mchakato wa vikao vinavyoendelea vya kuchuja na kupata kiongozi atakae peperusha bendera ya chama cha mapinduzi, Huo ni wajibu wake akiwa ni mwenyekiti Wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa, na ndio muwakirishi Wa rais kwa ngazi ya mkoa anawajibu na kila sababu ya kukemea, kuonya, kushauri na kuelekeza mambo yote yanayohusu raia na Mali zao hivyo sisi wana mwanza na watanzania kwa ujumla hatukuona ubaya wa aina yeyote kwa kauli ya mkuu wetu wa mkoa.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Hussein. A. Kimu (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Wamachinga mkoa wa Mwanza Iddi Tembo (kulia) na mkuu wa kundi lisilo rasmi la mabaunsa mkoani Mwanza, Mbayi Kambarage (kushoto)
Wanahabari kikazi zaidi.
Cha kusikitisha Jana 7/7/2015. Kuona katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari mtu
anae jiita mtemi Sylvester Yared, ambae ndiye mratibu Wa genge la vijana wahuni wanaojiita 4U movement. Akidhihaki na kupinga tamko la mkuu wetu Wa mkoa wa Mwanza. Binafsi nilishitushwa sana.....
Katika Katiba yetu ya chama cha mapinduzi na kanuni zake tuna jumuiya tatu 1.Jumuiya ya wanawake(UWT) 2.Jumuiya ya wazazi 3.Jumuiya ya vijana (UVCCM) Ndani ya chama cha mapinduzi hatuna taasisi wala jumuiya inayoitwa 4Umovement. Swali la kujiuliza jeuri, kiburi na mamlaka ya kuunda chombo kisicho rasmi chenye lengo la kuvuruga,kuhatarisha mustakabari wa chama chetu na Taifa letu kwa maslahi ya mtu binafsi,anaetumia kundi la vijana wasio jitambua kwa gharama yeyote ili aingie ikulu,na huyu si mwingime bali ni ndugu Edward Lowasa.
Ninayaongea haya kwa ushahidi, ninao hapa viongozi wawili kutoka kundi la mabaunsa na machinga, wa mkoa wa mwanza ambao walifatwa na kupewa kazi ya kuandaa na kukusanya vijana wasiojielewa kwa lengo la kwenda Dodoma. Kushinikiza viongozi Wa chama kumchagua mgombea wao, na kundi jingine la vijana na akina mama Wa CCM kusimama njiani kusimamisha misafara ya wajumbe Wa NEC, na mkutano mkuu wa chama Taifa kuwapa shinikizo na vitisho, kwamba lazima warudi na mgombea wao ndugu Edward Lowassa. 
Wanahabari kikazi zaidi.
Hayo yote yanafanywa kwa malipo, Na kila kijana atalipwa tsh 100,000.kwa kila siku ,kwa siku zote atakazo fanya kazi, mpaka kieleweke.
Ndugu wanahabari Mimi kijana mzalendo wa Tanzania ninapata wakati mgumu na Mashaka makubwa pindi ninapo ona mtu ambae hakubaliki katika jamii ya watanzania mwenye madoa na kashfa chungu nzima tena afya yake ikiwa ya kususua analazimisha kwa kutumia gharama kubwa ili afike Ikulu mtu huyu kwa kauli ya hayati baba Wa Taifa,namnukuu, Tumuogope kama ukoma hafai.mwisho wa kunukuu.
Nimalizie kwa kuwashukuru na kuwapongeza viongozi wetu wakuu wa chama na serikali kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kujenga na kuimarisha chama na serikali kwa kutatua na kusimamia maslah ya watanzania, Mwisho kwa nafasi ya kipekee niwashukuru wanahabari wote mlio hudhuria na watanzania wote mnao nisikiliza na kunitazama.Mungu kibariki chama chetu CCM, Mungu ibariki Tanzania.
Imeandaliwa na Hussein. A. Kimu Mw/kiti UVCCM(W) Nyamagana Mwanza.
Tupe maoni yako

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post