Na Joseph Ngilisho
MFANYABIASHARA wa Nyama ,Godson Rwaichi (24),mkazi wa Eso jijini
hapa .amenusurika kuuawa baada ya watu wasiofahamika kumimimia risasi
nane maeneo mbalimbali ya mwili wake.
Akizungumza kwa tabu akiwa amelazwa katika chumba cha watu mahututi
(ICU),Seliani jijini Arusha alisema watu hao walimvamia juzi majira ya
saa mbili usiku baada kumwita katika nyumba moja wapo eneo hilo
Alisema hakuweza kuwatambua watu hao kwani mara baada ya kufika katika
nyumba hiyo alishangaa kuona watu wakiteremka kwenye gari na moja wapo
alimiminia risasi nane zilizo mjeruhi tumboni ,Mkononi ,Mguuni
,Mapajani na maeneo mengine ya mwili.
Aliongeza kuwa kitendo hicho kilimfanya anguke chini na kuzimia na
baadae kujikuta akiwa hospitalini akipatiwa matibabu kwa lengo la
kuokoa maisha yake
Naye kaka wa majeruhi huyo, Daudi Rwaichi alisema kuwa tukio la
kushambuliwa kwa mdogo wake limetokea katika mtaa wa kanisani Paloti
na kwamba walitoa taarifa polisi na mtu moja mwanamke alikamatwa kwa
mahojiano
Hata hivyo alieleza kuwa hadi sasa badi hawaja fahamu chanzo cha
mdogo wake kushambuliwa kwa risasi kwani hakuwai kuwa na ugomvi na mtu
yeyote na wanasikitishwa na unyama ulio fanywa na watu hao ambao hadi
hivi sasa hawajafahamika
Aidha amelalamikia jeshi la polisi kwa kushindwa kufatilia kwa undani
tukio hili kuweza kuwatia mbaroni wahusika ambao baadhi watu alidai
kuwafahamu.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatusi Sabasi alidhibitisha
kutokea kwa tukio na kudai kuwa uchunguzi unaendelea
Hali ya mfanya biashara huyo bado ni mbaya kwani hadi sasa bado
anapumua kwa msaada wa mashine alizoekewa huku ndugu wakiendelea
kumwomba mungu aokoe maisha ya ndugu yao ,