ZOEZI LA UANDIKISHAJI BVR WASIMAA KWA SAA 3


Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura  (BVR)
katika kituo cha kujiandikisha cha shule ya Msingi Kiwawa kata ya
Imbaseny  wilaya ya Arumeru limesimama kwa muda wa saa tatu kutokana
na tatizo la kukosekana kwa wino jambo liliosababisha msongamano
mkubwa wa watu na kulalamikiwa na watu wengi.

Wananchi wa kata hiyo Epifania Sibula na Gorge Kavishe wamelalamikia
zoezi hilo kuwa na hitilafu zinazoweza kutatulika ambazo zinakwamisha
zoezi hilo na kuokoa muda badala ya watu kushinda vituoni wakafanye
shughuli za uzalishaji.

Epifania Sibula alisema kuwa alishinda kituoni hapo tangu jana jioni
bila mafanikio na kurudi leo ambapo amekutana na masaibu ya zoezi hilo
kusimama kwa masaa matatu jambo ambalo linamkatisha tama ukizingatia
idadi kubwa ya watu waliofika kituoni hapo kujiandikisha.

“Tumefika hapa saa 2 asubuhi lakini cha kushangaza waandikishaji
wamekuja saa 3:30 asubuhi hawazingatii muda mamia ya watu wanasubiri
huduma na bado  mchana majira ya saa 8:20  mchana  hadi saa 10:42
hapa wino umeisha  kama unavyoona tumesubiri sasa hivi ndo wameleta
wino zoezi linaendelea” Alisema Sibula

Sibula amesema kuwa tangu kuanza kwa shughuli za uandikishaji shughuli
za uzalishaji zimesimama kutokana na dosari ndogo ndogo ambazo
husababisha watu kukaa muda mrefu vituoni na wengine kukesha kwasababu
hakuna mashine za kutosha,wino na wakati mwingine mashine kufanya kazi
taratibu.

Geoge Kavishe alisema kuwa serikali iongeze mashine za kutosha katika
vituo vyenye idadi kubwa ya watu ili kuepuka migogoro inayoweza
kutokea katika vituo vya uandikishaji.

Ameitaka serikali kuongeza siku zaidi ili wananchi wote wapate fursa
ya  kujiandikisha ikiwemo kinamama ambao hushindwa kushinda katika
vituo vya kujiandikisha kutokana na majukumu ya malezi ya watoto
wadogo waliyonayo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post