Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu na aliyepata kuwa kada wa Chama cha Mapinduzi, Edward Lowassa atangaza rasmi kukihama Chama Cha Mapibnduzi (CCM) na kujiunga na Chama Kikuu cha Upinzani cha Chadema hii leo.
Lowassa ametangaza rasmi hii leo na kueleza namna mchakato mzima wa kumpata mgombea wa CCM ulivyo kuwa.
Lowassa na mkewe wamekabidhiwa kadi zao za uanchama hii leo mbele ya viongozi wa vyama vya upinzani vya CUF,NLD na NCCR Mageuzi na matangazo hayo yanaoneshwa moja kwa moja na Azam TV pamoja na ITV.