Usili
wa kwanza wa Dance 100% (2015) umefanyika kwa mafanikio makubwa Temeke
jijini
Dar es Salaam, ambapo makundi ya Team ya Shamba, The WT Group, WD, The Best
Boys Kaka Zao na Team Makorokocho wameweza kushinda nafasi ya kuingia katika
michuano kutoka wilaya ya Temeke.
Makundi
haya yamechuana vikali na mengine 6 yanayokamilisha idadi ya makundi 11,
UNI 6
Crew, GMF Crew, TWC, Dar Crew, Noma Sana Crew, na Viga Stars yaliyojitokeza
kuwania nafasi hiyo katika usajili huo wa kwanza.
Mratibu
wa mashindano hayo kutoka East Africa Television na East Africa Radio, Bi
Happy
Shame, amesema kuwa amefurahishwa na utulivu na amani ambayo wapenda
burudani
Temeke wameonyesha leo, huku pia kukiwa na vipaji mbalimbali kutoka makundi
yaliyojitokeza katika usaili huo wa kwanza.
Akizungumza
baada ya kumalizika michuano ya usaili huo, mratibu wa Dance 100% kutoka
BASATA, Kwerugira Maregesi, mbali na kufurahishwa na vipaji vilivyojitokeza,
amekumbushia umuhimu wa makundi hususan yale yanayotarajiwa kushiriki
usajili
unaofuata, kuzingatia vigezo na masharti yaliyowekwa kujiwezesha kushinda,
ikiwepo ubunifu katika mitindo ya kudansi, kuburudisha na muonekano, huku
akishauri kupunguzwa kwa mitindo ya sarakasi na kuongezwa ladha katika
upande
wa dansi zaidi.
Majaji
Super Nyamwela, Queen Darleen na Shetta wametumia umakini nkubwa kuhakikisha
wanatoa alama zinazostahili kwa mujibu wa vigezo kwa washiriki wote, huku
burudani mbalimbali zikijiri zikishereheshwa kikamilifu na watangazaji
rasmi wa
Dance 100 kwa mwaka huu, T-Bway 360 na mrembo Maggie
Vampire.
Majaji
pia kila mmoja kwa nafasi yake wametaka washiriki watakaoendelea kujitokeza
kujipanga zaidi wakizingatia vigezo vilivyowekwa, ambavyo ndivyo
wanavyovitumia
kutoa maksi (alama) zitakazowawezesha kufikia
ushindi.
Usajili
wa pili wa mashindano haya makubwa kabisa ya kudansi utafanyika katika
viwanja
vya Don Bosco Upanga siku ya Jumamosi Tarehe 01 Agosti 2015, ambapo makundi
mengine matano yatasakwa kushiriki katika michuano hiyo kwa mwaka
huu.
Usikose
kujionea kwa urefu yote yaliyojiri pale TCC Chang'ombe katika
mashindano ya
usajili huo, kwa kutazama ting'a namba moja kwa vijana EATV, siku ya
Jumamosi, kuanzia
saa 12 na nusu jioni.
East
Africa Television na East Africa Radio inaleta Dance 100% kwa kupewa nguvu
na
mtandao wa Vodacom Tanzania na Coca Cola ambao ndio kinywaji rasmi cha dance
100% (2015).
PICHANI
JUU: Kati ya makundi matano yaliyopita kwenye usaili wa kwanza wa
Dance 100% (2015) - Temeke. Kundi linaitwa 'The Best Boys Kaka
Zao'
Kutoka
kushoto -Majaji wa mwaka huu kwenye Dance 100% ni Super Nyamwela,
Shetta na Queen Darleen wakiwa wanajumulisha matokeo ya washiriki kutoka
Temeke.
Shabiki
wa kundi la 'Noma Sana' akiwa anajitayarisha kushangilia timu yake kwenye
usaili wa kwanza Temeke kwenye Dance 100% (2015)
Washiriki
wa kundi la 'Noma Sana' mwaka huu kwenye Dance 100% wakiwa wanafanya yao
viwanja vya TCC Changombe.
Watangazaji
rasmi wa Dance 100%, TBway 360 na Maggie Vampire wakiwa wanasherehesha
kikamilifu huku burudani mbalimbali zikijiri TCC Changombe.