BREAKING NEWS

Thursday, July 16, 2015

MICHMICHUANO YA STERLING PRO- TOURNAMENT YASHIKA KASI ARUSHA

Mashindano ya gofu kwa wachezaji wataalamu yameendelea kushika kasi katika
viwanja vya gymkhana jijini Arusha,baada ya jumamosi hii kuchezwa.


Mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya Sterling Surfactants limited
Arusha hufanyika kila mwezi ambapo wataalamu hao huchuana vikali  .


Katika michuano iliyomalizika jumamosi ,Nuru Mollel ameendelea kuonyesha
umahiri wake baada ya  kujipatia jumla ya pointi 55 .5 kwa muda wa miezi
mitano tangu kuanza kwa mashindano hayo .


Anafuatiwa na  Jimmy Mollel ambaye naye amejikusanyia jumla ya pointi
43.5,huku  John Leonce akijikusanyia jumla ya pointi 28.5. Elisante Lembris
akijikusanyia jumla ya pointi 19.5  Miezi mitano sasa.


Akizungumzia ushindani anaoendelea kuuonyesha katika michuano hiyo Nuru
Mollel alieleza kuwa mtarajio yake ni kuhakikisha anaendelea kufanya vizuri
hadi miezi 12 inakamilika ili aweze kuwa mshindi.


Michuano hiyo hufanyika kila mwezi ambapo baada ya miezi 12 , mwenye pointi
nyingi atajipatia zawadi kiasi cha shilingi milioni moja na mshindi wa pili
atapata shilingi laki sita.


Mbali na michuano ya Sterling pro- tournament, Pia  klabu ya Arusha Golf
gymkhana iliendelea na mashindano yake ya kila mwezi  yanajulikana kama PAL
GUPTA MOUNTHLY MUG  ambayo  yalishirikisha jumla ya wachezaji 36 .


Washindi mbalimbali walipatikana ambapo Division A  Richard Gomes alipata
72 nett na mshindi wa pili kuwa ni Raju Lodhia aliyepata 74 nett, huku
katika Divisioni B Dave Mullican alipata  71 nett  na kufuatiwa na hitten
Nathwani kwa 71 na Division C Perfect Lymo alipata  79 nett na mshindi wa
pili kumwendea Haja Modhwadia kwa 81 nett.


Aidha klabu ya Arusha Golf Gymkhana inatarajiwa kufanya mashindano ya wazi
ya mchezo huo (The Arusha golf Open Competition) yanayotarajiwa kufanyika
kwa siku mbili tarehe 25 na 26 ya mwezi july  mwaka huu katika viwanja vya
Gymkhana jijini Arusha.


Mashindano hayo  ya wazi yatashirikisha  julma ya wachezaji 80 kutoka
maeneo mbalimbali nchini ambayo ni  pamoja na Dar es salaam gymkhana
lkabu,Lugalo golf klabu, Moshi golf Klabu, TPC golf klabu na Morogorogolf
klabu. kwa mijibu wa competition Manager klabu ya Arusha Gymkhana Shakiri
Bandali.


Akizungumzia mashindano hayo  ya wazi kocha wa timu ya taifa  ya ya mchezo
wa Gofu, Olais Mollel alisema mashindano hayo yana lengo la kunyanyua
vipaji  vya wachezaji kwa ajili ya kujiandaa kuchagua timu ya taifa hapo
baadae.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates