Ticker

6/recent/ticker-posts

LOWASA AKARIBISHWA CHADEMA

Mwanachama wa CHADEMA Monduli mjini  akiwa ambeba bango lenye ujumbe
unaoashiria kumkaribisha Edward Lowassa katika chama hicho,jana katika
mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Monduli Mjini.Picha na
Ferdinand Shayo



Siku chache baada ya Lowasa kuenguliwa kwenye kinyang`anyiro cha
Uraisi kwa tiketi ya CCM,jana CHADEMA imezuru katika jimbo hilo na
kufanya mkutano wa hadhara  ambapo wamepokea wanachama wapya 10
waliojiunga kutoka CCM.

Katika Mkutano huo uliobeba ujumbe wa Kumkaribisha Lowasa katika chama
hicho kwani bado milango haijafungwa kwa yeye kutimiza azma yake ya
kuwatumikia watanzania walio wengi

Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA)
,Happiness Chale alisema  kuwa uamuzi mbaya walioufanya CCM Lowassa
hana budi kujiunga na CHADEMA mapema kabla milango haijafungwa ili
aweze kufanikisha azma yake ya kuwatumikia Watanzania.

“Saa ya ukombozi imefika wananchi wa Monduli wajiunge na chadema ili
kuleta mabadiliko na ukombozi wa kweli walioukosa kwa muda mrefu”
Alisema Happiness

Katibu wa BAWACHA ,Cecilia Ndossy ambaye pia ni Mtia nia katika jimbo
la Monduli amesema kuwa  kwa kosa walilolifanya CCM hawapaswi kupewa
ridhaa ya kuongoza wananchi hao badala yake wachague chadema mahali
ambapo sauti ya watu inaheshimiwa na kupewa kipaumbele.

Cecilia amejizatiti kuhakikisha kuwa anaboresha huduma za afya,maji
safi na salama na miundombinu kwani jimbo hilo linakabiliwa na uhaba
mkubwa wa maji kwa muda wa miaka mingi.

Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Monduli  Japhet Sironga amewakaribisha
watu wa Monduli kujiunga na chama hicho kinachothamini matakwa ya watu
wengi na si ya baadhi ya watu wachache kama ilivyo kwa chama tawala.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Diwani wa kata ya Sombetini Ally
Bananga amesema kuwa anaamini kuwa Lowassa ameondolewa vitani ila
hajashindwa mapambano hivyo ana nafasi ya kushinda.

Mwenyekiti  wa BAWACHA wilaya ya Arusha ,Viola Lazaro amewataka
wananchi wa Monduli  wa  Monduli wajitokeze kwa wingi katika zoezi la
uandikishaji ili wapate haki ya msingi ya kuchagua viongozi makini
watakaoeleta maendeleo ya Monduli na taifa kwa ujumla

Post a Comment

0 Comments