Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akishuka kwenye ndege mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Singida.
Mh. Mohammed Dewji akilakiwa na Mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida, Hassan Mazala mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Singida mjini kwa ajili kuhutubia Mkutano mkubwa ambao atawasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya mwaka 2005/2010 na 2010/2015 ambapo Mwanamuziki wa kimataifa Nassib Abdul almaarufu kama Diamond Platnumz atatumbuiza wanaSingida. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya Singida, Jumanne Hamis Nguli.
Mh. Mohammed Dewji akisalimiana na Katibu wa CCM wilaya ya Singida mjini, Magdalena Ndweta.
Mh. Mohammed Dewji akisalimiana na Katibu ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya Singida mjini, Duda Juma.
Mwanamuziki wa kimataifa nchini, Diamond Platnumz akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya Singida, Jumanne Hamis Nguli.
Mh. Mohammed Dewji akionekana mwenye furaha na tabasamu bashasha akiongoza na Mwenyekiti wa CCM wilaya Singida, Jumanne Hamis Nguli kusalimiana watoto na wananchi waliojitokeza kumlaki katika uwanja wa ndege wa Singida mjini.
Umati wa watoto wanaoishi karibu na maeneo ya uwanja wa ndege wa Singida mjini wakiwa wamefurika kwenye uwanja huo kumpokea mbunge wao.
Pichani juu na chini watoto na vijana wakimfurahia Mbunge wao Mh. Mohammed Dewji.
Diamond Platnumz akigombaniwa na wakazi wa Singida mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Singida.
Mwanamuziki wa kimataifa Diamond Platnumz, Rommy Jones pamoja na mlinzi wake wakielekea kwenye gari maalum mara tu baada ya kuwasili.
Wananchi wa Singida mjini wakimsindikiza Mbunge wao Mh. Mohammed Dewji.
CCM Oyeeeeeeee!!!