MBARONI KWA KUMUUA KWA PANGA MFANYABIASHARA
MKAZI
wa kijiji cha Mgombani ,wilaya ya Monduli Mkoani Arusha, Juma Ndaji(27)
, anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo kwa kosa la kumkata
panga mfanyabiashara ,Paulo Akwesso(58) na kumsababishia kifo chake
akimtuhumu kuwa na mahusiano na mpenzi wake.
Aidha
mtuhumiwa huyo pia alimjeruhi kwa panga mwanamke Rebeka John
(22)anayedsiwa kuwa ni mpenzi wake ambaye elazwa katika kituo cha Afya
Mto wa mbu kwa matibabu,baada ya kumkuta na marehemu wamelala kitanda
kimoja.
Akiongea na
waandishi wa habari Mkuu wa wilaya ya Monduli Frank Mwaisumbe alisema
kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa nne usiku katika kitongoji
cha Kirurumo, kata ya Majengo,katika chumba cha mwanamke huyo.
Akifafanua
kuwa chanzo cha tukio hilo ni mtuhumiwa kumtuhumu marehemu kuwa na
mahusiano na mpenzi wake ambaye pia alijeruhiwa kwa panga baada ya
kuwakuta wakijivinjari chumbani.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Migombani ,Festo Philpo alisema kwamba mara baada ya
kupata taarifa za tukio hilo alifika katika chumba cha Rebeka na kukuta
polisi wakimhoji mtuhumiwa ambaye alikiri kuhusika kumshambulia marehemu
na kumsababishia umauti.
Mwenyekiti huyo akifafanua kuwa marehemu alikuwa akifanyabiashara ya kuuza vinywaji huku Rebeca akiwa mfanyakazi wake.
Alisema
kuwa awali mtuhumiwa alikuwa na mahusiano na Rebeca lakini walitengana
kitambo, hivyo hatua ya kuwenda kuwashambulia kwa Panga ni kutokana na
wivu wa mapenzi.
Alisema
kuwa mtuhumiwa alipata taarifa kuwa Marehemu amekuwa akienda kstika
chumba cha Rebeka na kulala ndipo alipoamua kumvizia usiku akiwa na
panga mkononi na kufanikiwa kuwakuta.
"Mtuhumiwa
alifika katika chumba cha Rebeka na kumkuta marehemu akiwa chumbani na
kuanza kumkata na panga na kuwajeruhi wote wawili lakini marehemu Paulo
alivuja damu nyingi sana na kufariki dunia akipatiwa matibabu katika
kituo cha afya mto wa mbu ''Alisema
Alisema
marehemu alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika kituo cha
Afya Mto wa Mbu baada ya kuvuja damu nyingi na polisi inamshikilia
mtuhumiwa kwa kusababisha kifo cha marehemu.
Hata
hivyo aliongeza kuwa mtuhumiwa baada ya tukio hilo alijitahidi kuficha
Panga kwa kulitupa kwenye shamba la migomba, lakini polisi walifanikiwa
kulipata likiwa katikati ya mgomba likiwa na damu mbichi.
Mwili
wa marehemu umehifadhiwa katika kituo cha Afya Mto wa Mbu ukisubiri
uchunguzi wa daktari ,mtuhumiwa ambaye anashikiliwa polisi atafikishwa
mahakamani kujibu tuhuma za mauaji zinazomkabili.

0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia