Na Woinde Shizza, wa libeneke la kaskazini blog
Mtuhumiwa
mauaji ya kutisha ya kumkata viungo vya mwili marehemu zikiwemo sehemu za siri,
viganja vya mikono na matiti mauaji yaliotokea kwenye hotel ya A Square Belmot
amekamatwa na jeshi la polisi mkoani hapa.
Akiongea na vyombo
vya habari ofisini kwake kamanda wa polisi, Naibu kamishna wa jeshi la polisi
mkoani hapa Liberatus Sabas alisema kuwa mtuhumiwa alikamatwa juzi majira ya
asubuhi katika eneo la TRA House jijini hapa.
Sabas
alisema kuwa alipohojiwa na polisi alikiri kushiriki mauaji hayo na ndipo alipowapeleka
kuwaonyesha polisi alipovitupa viungo vya marehemu eneo la mto misheni usa
river nje wilayani meru.
Alisema kuwa
marehemu ametambuliwa jina kamili Alfred Kimbaa mwenye umri wa miaka18 mkazi wa
mianzini jijini hapa huku mtuhumiwa ambaye jina lake limetambuliwa kwa Elijus
Lyatuu mkazi wa Dar es Salaam ambaye marehemu alikuwa akiuza duka la kaka yake
alietambuliwa kwa jina moja la Lyatuu anaeishi jijini Dar es salaam.
Alisema kuwa
mtuhumiwa ni mwanafunzi wa mwaka wa tano chuo cha falsafa cha kanisa katoliki
Segerea na alipofika Arusha kwa mara ya kwanza aliishi na marehemu chumba
kimoja kabla ya mgogoro kuanza na ndipo alipofikia kumuua marehemu na kuiacha
maiti yake katika hotel nae kutokomea kusikojulikana hadi alipokamatwa juzi.
Alisema kuwa
mtuhumiwa Elijus alimua marehemu kwanza kabla ya kuanza kucharanga viungo ndio
maana chumbani alikokutwa marehemu hakukua na damu.
“Tukio hili
lisihusishwe na imani za kishirikina kwani kulikuwa na mgogoro kati ya
mtuhumiwa na marehemu uliopelekea mtuhumiwa kufanya tukio hilo”alisema Kamanda
Sabas
Upelelezi
ukikamilika na taratibu za jeshi la polisi zinaendelea na zikikamilika mtuhumiwa
atafikishwa mahakamani.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia