Bw.
Karl Heinz Knoop akielezea historia fupi kuhusu kampuni yake kwa
wanafunzi wa Chuo cha kumbukumbu ya Mwl. Nyerere akiwemo Miss Ilala 2013
Dorice Mollel wanaoshiriki program ya mwezi mmoja nchini Ujerumani.
Miss
Ilala 2013 Dorice Mollel (kushoto pichani) akiwa kwenye program ya
mwezi mmoja, na wenzake 8 kutoka Chuo cha kumbukumbu ya Mwl. Nyerere
ambapo wamepata nafasi ya kwenda kutembelea Kiwanda cha Kilimo
kilichoanzishwa mwaka 1972 ambacho kinamilikiwa na Bw. Karl Heinz
Knoop , mwenye uzoefu wa miaka 50 ambaye anatarajia kujenga kiwanda hiki
pia nchini Tanzania mkoani Kilimanjaro Moshi kitakachofahamika kwa jina
la Reila amabavyo pia vipo zaidi ya nchi 11 duniani na kwa Afrika ni
Tanzania pekee tumepata bahati hiyo ya kuletewa Teknlolojia anayotumia
ya kutengeneza umeme wa gesi na pia kutunza mazao, hii itasaidia sana
kukuza sekta ya kilimo Tanzania.
Dorice
Mollel amesema “ hichi ni kitu cha muhimu sana nikiwa kama mrembo
nikirudi nyumbani na kuieleza jamii inayonizunguka ili kutuletee faida
baadae nchini kwetu”.