Ticker

6/recent/ticker-posts

MFANYAKAZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI(MUWSA)AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI .


Pikipiki aina ya Suzuki ikiwa imenasa mbele ya Lori baada ya kugongana uso kwa uso .
Baada ya ajali hiyo pikipiki ilibaki ikiwa imesimama baada ya kunasa chini ya Lori la mafuta.
Mwili wa marehemu George Lyamuya ukiwa pembeni baada ya kugongwa na lori la mafuta.
Askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiwa katika eneo la tukio kwa ajili ya kufanya vipimo.


Ajali mbaya imetokea barabara kuu ya Arusha Moshi ikihusisha Lori aina ya Sacania lenye namba za Usajili T 137 ATA na pikipiki aina ya Suzuki yenye namba SU 40262 mali ya Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA).

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo waliiamia globu ya jamii kuwa ilitokea majira ya saa 7 katika makutano ya barabara ya Arusha/Moshi na ile itokayo chuo cha polisi Moshi kuelekea ofisi za mkuu wa wilaya ya Moshi.

Katika ajali hiyo dereva wa Pikipiki aliyefahamika kwa jina la George Lyamuya ,mfanyakazi wa Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi alufariki dunia papo hapo.

Post a Comment

0 Comments