Mkuu wa Wilaya ya Longido, James Ole Millya
Kundi la tembo limevamia makazi ya wananchi wa Kata
ya Tingatinga, Wilaya ya Longido, mkoani Arusha na kusababisha kifo cha
mtu mmoja na mwingine kujeruhiwa.
Katika hekaheka ya kukabiliana na tukio hilo, tembo mmoja ameuawa kwa ushirikiano wa wananchi na askari wa wanyamapori kutoka Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Kaskazini.
Wananchi wa kata hiyo, waliliambia LIBENEK kuwa aliyeuawa na tembo hao ni mtoto wa miaka tisa aliyetajwa kwa jina la Fred Joseph, huku Paulo Lukari, akijeruhiwa na kulazwa hospitali.
Wakizungumza baada ya Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Kaskazini kufika na kushirikiana nao kumuua tembo aliyesababisha madhara hayo, wananchi hao wamelalamikia watendaji wa sekta ya wanyamapori kwa kuendelea kukaa mijini na kusubiri kupewa taarifa wakati wananchi vijijini wakiendelea kuuawa.
Diwani wa Kata ya Tingatinga, Sabore Olemoloimet, ameiomba serikali kuhakikisha watendaji wanaoshughulikia migogoro ya wananchi na wanyamapori kuhamia maeneo husika ili wawadhibiti wanyama kabla hawajaleta madhara.
“Kuna haja ya watendaji wa sekta hii kuwa karibu na wananchi, hasa kwenye maeneo hayo, ambayo yamekuwa yakilalamikiwa kila siku na wananchi, kwani pamoja na umuhimu wa wanyamapori tatizo hili linawaongezea wananchi umaskini,” alisema Sabore Olemoloimet, ambaye ni Diwani Kata ya Tingatinga.
Mkuu wa Wilaya ya Longido, James Ole Millya, alithibitisha kuwapo kwa udhaifu mkubwa kwa watendaji wanaoshughulikia wanyamapori na kwamba, licha ya kutoa maelekezo mara kadhaa bado hayafanyiwi kazi.
“Nimeshamwandikia mkurugenzi barua, lakini naona bado hajachukua hatua. Itabidi nichukue hatua zaidi kwa ngazi za juu,” alisema Millya.
Baada ya tembo huyo kuuawa, makundi ya wananchi wa eneo hilo yalifika na kuanza kugawana kitoweo, huku wakimshukuru Mungu kwa kuwawezesha kuondokana na tatizo hilo na pia kupata kitoweo.
Baadhi walitaka wapewe kipaumbele kwa kupewa nyama nyingi kwa madai kuwa wameathirika zaidi na wanyama hao.
Vilio vya wananchi juu ya madhara yanayosababishwa na wanyamapori, wakiwamo tembo vimekuwa vikisikika katika kona mbalimbali nchini jambo linaloonyesha kuwa bado tatizo hilo halijapata ufumbuzi wa kudumu.