wananchi wa mitaa ya Kingereka na Kibaoni katika kata ya Hai
Mjini wakimsikiliz a mkuu wa wilaya ya hai katika mkutano wa hadhara .
Na Mwandishi Wetu,Mwangulube,Hai
Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga ameeleza
kuwa serikali wilayani humo imejipanga kuondoa kero zote zinazoawakabili
wananchi wanapoenda kutibiwa katika hospitali ya serikali ya wilaya hiyo
zikiwemo lugha chafu za watumishi wa hospitali hiyo
Makunga ametoa kauli hiyo katika mikutano yake
ya hadhara na wananchi wa mitaa ya Kingereka na Kibaoni katika kata ya Hai
Mjini.
Awali wananchi wa mitaa hiyo walieleza kuwa kero
kubwa wanayokumbana nazo katika hospitali hiyo ni pamoja na lugha chafu katika
eneo la mapokezi,ukosefu wa dawa pamoja na madaktari kutokaa katika vyumba vyao
vya kuwahudumia wagonjwa.
Mkuu huyo wa wilaya ameeleza kuwa hatua za awali
zimeshaanza kuchukuliwa ikiwemo kuanzisha mpango unaojulikana kama sauti ya jamii ambapo
kupitia mpango huo wananchi wanaokumbana na kero katika hospitali hiyo wamekuwa
wakitoa taarifa.
mkuu wa wilaya ya hai Novatus Makunga akiongea na wananchi wa mtaa wa kingereka
"Taarifa
hizo zimekuwa zikijadiliwa na kamati ya uongozi ya hospitali hiyo kila
mwezi na kuchukuwa hatua na baadaye mrejesho kutolewa kwa wananchi,hivyo
zote kwa pamoja tupambane na uvunjaji wa maadili katika hospitali yetu"
alisema Makunga
Aidha amewataka wananchi hao kutoa taarifa mara
moja pale wanapokumbana na kero yoyote kwa mganga mkuu wa wilaya ama mganga
mfawidhi ama muuguzi mkuu na hata yeye kama mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ambapo wote hao walitoa nambari zao za simu za mkononi.
“Tumeanza kuchukuwa hatua na itakuwa vyema pale
unapokumbana na kero kutuletea taarifa hapo hapo bila ya kuchelewa,sasa wakati
umefika wa kuambiana ukweli,kama mtu anaona kuhudumia umma kunampotezea wakati
basi akaanzishe zahanati yake ambapo huko atakuwa huru kutumia lugha chafu,”aliongeza
Makunga
Ameeleza maboresho makubwa yaliyofanywa na
serikali katika hospitali hiyo hayatakuwa na maana endapo kero hizo zitaendelea
kudumu na kusababisha wananchi kupata huduma kwa mateso makubwa.
Makunga amezitaja huduma zilizoboresha kuwa ni
pamoja na upasuaji mkubwa kwa kuwa na chumba cha kisasa,ukamilishaji wa wote ya upasuaji pamoja na kukamilishwa kwa
huduma za X-Ray ambayo itafunguliwa rasmi na mwenge wa uhuru mnamo tarehe 22
ya mwezi huu
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa wilaya ya
Hai,Dk Fanuel Mollel alikiri kwamba huko nyuma kulikuwa na tatizo kubwa la
madaktari wa hospitali hiyo kutumia muda mrefu kwenda kunywa chai kwa kutoka
pamoja kwa makundi na hivyo kusababisha wagonjwa kusota kwa muda mrefu.
Amesema hatua za kudhibiti tabia hiyo
zimeshachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuanzisha kantini eneo la hospitali hiyo.
Kuhusiana na upungufu wa dawa ameeleza hali hiyo
inatokana na taratibu za serikali ambapo kwa sasa zinataka dawa ziagizwe kutoka
katika bohari kuu ya madawa(MSD) ambapo mara nyingine ukumbwa na upungufu wa
dawa