Ofisa masoko wa shirika la Farm Africa, Rahel Pazzia (kulia) akiwa
na baadhi ya wakulima wa ufuta wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara jana, katika
banda la Farm Afrika kwenye maonyesho ya wakulima nane nane kanda ya kaskazini,
yanayofanyika viwanja vya Themi jijijni Arusha.
Watanzania wenye asili ya bara Asia wakipewa maelezo ya ubora wa
mafuta ya ufuta kwenye banda la shirika la Farm Africa, katika maonyesho ya
wakulima nane nane kanda ya kaskazini, yanayoendelea kwenye viwanja vya Themi
jijini Arusha.
Wakulima
wametakiwa kutumia fursa ya kuongeza thamani mazao yao ili waweze kunufaika zaidi
kiuchumi kuliko kuuza mazao yao yakiwa ghafi kwani watakuwa wanayonywa na
kuzidi kuwa masikini.
Wito
huo umetolewa jana na Ofisa masoko wa shirika la Farm Africa, Rahel Pazzia,
wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwenye maonyesho ya wakulima nane
nane, kanda ya kanda ya kaskazini yanayoendelea jijini Arusha.
Alisema
kupitia Farm Africa wakulima wengi wa ufuta wa mkoa huo wamenufaika kiuchumi kutokana
na kuongeza thamani mazao yao na kutouza yakiwa ghafi hivyo kujiongezea kipato
zaidi kinachowaletea maendeleo.
“Farm
Africa inawataka wakulima nchini waje wajifunze kupitia wakulima wetu wa ufuta,
hivi sasa wananufaika zaidi kiuchumi kwani badala ya kuuza ufuta, wanaongeza
thamani kwa kutengeneza mafuta, kashata, sabuni na kinywaji,” alisema Pazzia.
Alisema
wakulima sita wamefika kwa ajili ya kuonyeshaji mazao ya ufuta na misitu na
wakulima 45 wamekuja kujifunza kwa ajili ya kuongeza elimu zaidi na pia kutoa
elimu kwa wakulima wengine ili wajifunze kupitia wao.
Naye,
Ofisa miradi wa misitu na masoko wa shirika hilo, Hakam Mohamed alisema wanavijiji
33 wa wilaya ya Mbulu na Babati mkoani Manyara, wananufaika kupitia msitu Nou na
lengo lao ni kuijengea jamii uwezo zaidi wa kiuchumi.
Mohamed
alisema ili kuhakikisha jamii haiharibu msitu huo kwa kuutumia kwa matumizi
yasiyo ya mazuri wamebuni miradi ya kurina asali, miche ya miti, kulima uyoga
na ususi wa vikapu, ambayo imewanufaisha wote wanayozunguka Nou.
Mkulima wa ufuta wa Kijiji cha Ngolei Wilayani Babati Mkoani
Manyara, Costante Martin, akiwa na zana ya kilimo iitwayo Coster Planter, ambayo
aliibuni mwenyewe kwa kuwezeshwa na shirika la Farm Africa, hapa akiwa kwenye la Farm Africa katika
maonyesho ya kilimo nane nane kanda ya kaskazini, yanayofanyika viwanja vya
Themi jijini Arusha.
Ofisa miradi na masoko wa shirika la Farm Africa, kwa upande wa msitu
wa Nou unaowanufaisha wakazi wa vijiji 33 vya Wilaya za Babati na Mbulu
Mkoani Manyara, Hakam Mohamed akiwa
na Philemon Lawrent (kulia) wa Kijiji cha Boboa wilayani Mbulu na Joseph
Kufo wa Kijiji cha Bermy Wilaya ya Babati, wakiwa katika
banda la Farm Afrika jana, kwenye maonyesho ya wakulima nane nane kanda
ya kaskazini,
yanayofanyika viwanja vya Themi jijijni Arusha.
Emmanuel Stephano mkazi wa Kijiji cha Zeloto Wilaya ya Babati Mkoa
wa Manyara, hapa akiwa na miche aliyootesha kwenye banda la shirika la Farm
Africa, katika maonyesho ya kilimo nane nane kanda ya kaskazini, yanayofanyika viwanja
vya Themi jijini Arusha.
“Tumewawezesha
wawe na vicoba, wapate mikopo ili waweze kuibua miradi ambayo itawanyanyua
kiuchumi na kutokuwa na wazo baya la kuharibu msitu wa Nou ikiwemo kukata miti
kwa ajili ya kupata mbao,” alisema Mohamed.
Kwa
upande wake, mkulima wa ufuta wa kijiji cha Ngolei, Costantine Martin alisema
kupitia ufuta amenufaika kiuchumi kuliko kulima mahindi kwani gunia moja la
kilo 85 anauza sh215,000 huku gunia moja la mahindi likiuzwa sh30,000.
Naye,
mrina asali wa kijiji cha Boboa wilayani Mbulu, Philemon Lawrence alisema
kupitia shirika la Farm Africa, wameweza kujinufaisha kiuchumi kwa kuwezeshwa kupitia
miradi mbalimbali ikiwemo kupatiwa mizinga ya nyuki