Pichani ni Watoto wa marehemu Medard Kabikile Stima ambaye alikuwa ni Mweka hazina wa Manispaa ya Ilala wakiwa wamebeba msalaba pamoja na picha kuongoza kuingiza mwili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam ili kuangwa kiserikali na baadae kuelekea kanisani na kwenye makaburi ya Kinondoni ambapo leo Agosti 4, 2014 wamempumzisha katika nyumba yake ya milele.
Marehemu Stima alikufa katika ajali ya gari iliyotokea July 31, 2014 karibu na eneo la Bwawani, wakati wakielekea mjini Morogoro kwa shughuli za kikazi. Gari aina ya Landcluiser Mali ya Manispaa ya Ilala lilipasuka gurudumu la mbele hivyo likaacha njia na kugonga mti uliokuwa pembeni ya Barabara. Marehemu Stima alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Dereva anaendelea na matibabu.
Famili ya Marehemu Medard Kabikile Stima ambaye alikuwa ni Mweka hazina wa Manispaa ya Ilala akiwa na majonzi wakati wa kumuaga mpendwa wao katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Meya mpya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi akitoa heshima zake za mwisho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia akitoa heshima zake za mwisho.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa nae alikuwa mstari wa mbele kutoa heshima zake.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Raymond Mushi ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki akitoa heshima yake.
Waombolezaji wakitoa heshima zao za mwisho.
Kila mmoa alikuwa na sura ya majonzi.
Mwanamitindo Flaviana Matata alikuwa ni miongoni mwa waombolezaji.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Rugimbana (wa pili kulia) alikuwa ni mmoja ya waombolezaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia (Katikati) akiwa na viongozi wengine.
Mwanamitindo Flaviana Matata akimmfariji mke wa Marehemu Stima.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia akitoa heshima zake za mwisho.
Familia ya Marehemu Stima ikiongozwa na Mama Stima wakiwa na nyuso za majonzi.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Raymond Mushi ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki akitoa machache.
Meya mpya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi akitoa salamu za rambirambi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mwandisi Mussa Natty akitoa salamu za rambi rambi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akieleza wasifu wa marehemu Stima.
Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Elizabeth Nyambibo akieleza machache.
Msemaji wa Familia akitoa shukrani zake za pekee kwa watu wote walioweza kufanikisha maziko ya ndugu yao Marehemu Stima. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Tags
MATUKIO HABARI