Mgeni
Rasmi katika uzinduzi wa albamu ya muziki wa Injili ,Waziri Mkuu
mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akionesha albamu ya mwanamuziki nyota wa
muziki wa injili hapa nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la
yesu,mara baada ya kuizindua rasmi mbele ya maelfu ya washabiki na
wapenzi wa nyimbo hizo za kiroho ndani ya ukumbi wa Diamond
Jubilee,jijini Dar jana.
Waziri
Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akifungua kasha lenye CD, wakati
akizundua rasmi albamu ya mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa
nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,uzinduzi huo
umefanyika jana ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na
maelfu ya watu mbalimbali.Pichani kati ni Mkurugenzi wa Msama Promotions
Ltd,Bwa.Alex Msama sambamba na Mwimbaji nyota wa Injili,Rose Muhando
wakishuhudia tukio hilo.
Uzinduzi
huo ulioandaliwa na kampuni ya Msama Promotions,ulionekana kufana kwa
kwa kiasi kikubwa,huku waimbaji balimbali wakiwa wameshiriki onesho
hilo,lililokonga washabiki na wapenzi wa muziki huo kwa kiasi kikubwa.
Waziri
Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akisalimiana na mwanamuziki nyota wa
muziki wa injili hapa nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la
yesu,uzinduzi huo umefanyika jana ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee na
kuhudhuriwa na maelfu ya watu mbalimbali.
Baadhi ya Wadau wa Muziki wa Injili wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi huo uliofana kwa kiasi kikubwa.
Sehemu ya umati ya watu waliofika kwenye uzinduzi huo
Mwimbaji
wa nyimbo za Injili,Rose Muhanda akiwa na skwadi lake jukwaani
wakiimba mbele ya umati mkubwa wa watu (hawapo pichani),wakati wa
uzinduzi wa albamu yake mpya,uliofanyika katika ukumbi wa Diamond
Jubilee hapo jana,ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh
Frederick Sumaye.
Rose Muhando akiimba kwa hisia
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria uzinduzi huo
Mwimbaji wa nyimbo za Kiroho,Upendo Kilahilo,akiimba jukwaani.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Kenya,Sara K akiimba
Waziri
Mkuu Mstaafu,Mh Frederick Sumaye na wadau wengine wakishuhudia
yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo wakati wa uzinduzi wa albamu mpya ya
Rose Muhando iliyojulikana kwa jina la Shikilia Pindo la Yesu.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria onesho hilo.
Washabi na wapenzi wa muziki wa injili wakiendelea kushuhudia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi wa albamu ya Rose Muhando.
Palikuwa hapatoshi jukwaani
Mwimbaji John Lissu akiimba sambamba na skwadi lake
Mwenye kuguswa alijikuta akisimama na kuimba
Mwimbaji
mahiri wa nyimbo za Injili kutoka nchini Zambia Ephraim Sekelet akiimba
mbele washabi na wapenzi wa muziki huo,waliokuwa wamefurika ukumbini
humo.
Rose Muhando akiimba sambamba washabiki wake jukwaani