Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph
akipolewa na Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya
wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes alipofika shuleni hapo kukabidhi
msaada wa vitabu vya masomo ya Sayansi uliotolewa na Shirika la Read
International kupitia UNESCO.
Na Mwandishi wetu, Arumeru
Wanafunzi
wa shule ya Mwedo sekondari iliyopo wilayani Arumeru wamelishukuru
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kupitia Read
International la nchini Uingereza kwa kuweza kuwapatia vitabu vya kiada
vya masomo ya Sayansi hali itakayowafanya kupiga hatua katika masomo
hayo.
Akizungumza
kwa niaba ya wanafunzi hao Kaimu mkuu wa shule hiyo Clara Meijo alisema
kuwa kutokana na changamoto mbalimbali za masomo ya Sayansi
wanalishukuru Shirika la Read International kwa kuweza kuwapatia vitabu
hivyo tulivookabidhiwa na UNESCO.
Meijo
alisema kuwa shule hiyo ilianzishwa mwaka 2011 ikiwashirikisha
wasichana wa kimasai wanaoishi katika mazingira magumu wakiwa ni
wanafunzi waliokosa nafasi ya kupata elimu kwa kuwachukua wanafunzi
kutoka maeneo mbalimbali kwenye jamii ya kifugaji.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph
(kulia) akisalimiana na Mwalimu Clara Meijo mara baada ya kuwasili
shuleni hapo.
Aidha
alisema kuwa wanafunzi hao ni wale waliokuwa kwenye maeneo ambayo
upatikanaji wa elimu yalikuwa mbali, shule hiyo inayomilikiwa na Shirika
la Wanawake wa Kimasai (MWEDO) lenye makao makuu yake jijini Arusha
huku shule hiyo ikiwa imejengwa kwa michango mbalimbali ya wafugaji kwa
kutoa mifugo yao.
“Changamoto
kubwa inayoikabili shule yetu ni upungufu wa mabweni, maji na umeme wa
kudumu ikisababisha wanafunzi kushindwa kujianda kwa mitihani yao kwa
kujisomea nyakati za usiku hali inayoangusha ufaulu kwa wanafunzi hao”
alisema Meijo.
Ameiomba
Serikali na wafadhili kuwasaidia kupata umeme kwa haraka ilikuweza
kuongeza ufaulu na idadi ya wanafunzi huku akiomba pia kusaidiwa
upatikanaji wa maji safi kwenye shule hiyo na kuongeza kuwa msaada huo
wa vitabu umekuja wakati muafaka kwao na utasaidia kukua kwa ufaulu
shuleni hapo.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph
akisaini kitabu cha wageni shuleni hapo. Kulia ni Afisa Mradi wa uchumi
wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO
na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko aliyeambatana na Bw. Al Amin.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph
alisema kuwa wanaimani kubwa kuwa vitabu hivyo vitatumika kuongeza
uelewa kwa wanafunzi na kuwa vitabu hivyo vinatambuliwa na Wizara ya
Elimu katika kufundishia masomo ya Sayansi hivyo ni wajibu wenu kama
wanafunzi kujifunza kwa bidiii ili muwe mabalozi wazuri katika ujenzi wa
taifa.
Bw.
Al Amin aliongeza kuwa wanampango wa kuiboresha maktaba ya shule hiyo
kwa kuongeza matumizi ya Tehama kwa upatikanaji wa taarifa mbalimbali
kwa ajili ya masomo.
Shule
hiyo inawafanyakazi 18 wakiwemo walimu kumi na idadi ya wanafunzi
wakiwa 153 huku wanafunzi kumi ni wakutwa na waliobakia ni wa bweni.
Afisa
Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung
Su Ko akisaini kitabu cha wageni shule ya sekondari ya wasichana ya
Mwedo iliyopo wilayani Arumeru jijini Arusha.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph
(kulia) akizungumza na Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa
Shule ya wasichana ya Mwedo, Joseph Mangomes (wa pili kulia) wakati
akikagua maktaba ya shule hiyo kabla ya kukabidhi msaada wa vitabu vya
masomo ya sayansi vilivyotolea na Shirika la Read International kupitia
UNESCO. Kutoka kushoto ni Mwalimu Clara Meijo, Afisa Mradi wa Shirika la
Wanawake wa Kimasai (MWEDO) liliojenga shule hiyo Martha Sengeruan na
Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA,
Myoung Su Ko.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph
akitoa maelekezo ya namna ya upangiliaji wa vitabu kwenye maktaba hiyo
kwa Mwalimu wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya
Mwedo, Joseph Mangomes.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph
(wa pili kulia) akipitia rekodi za uhifadhi wa maktaba hiyo kabla ya
kuwaahidi kuleta Kompyuta itakayokuwa "Software" ya kisasa zaidi na
kuweza kuwarahisisha kuhifadhi na utunzaji wa kumbukumbu za maktaba
hiyo.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph
(kulia) akisikiliza maelezo ya mwanafunzi Evaline Gerald wa kidato cha
pili shuleni ya sekondari ya wasichana MWEDO anayesaidiana na Mwalimu
wake katika kutoa huduma za maktaba ya shuleni hapo.
Sehemu ya mashelfu ya kuhifadhia vitabu kwenye maktaba ya shule hiyo.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) na fisa
Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung
Su Ko wakipata maelezo ya maabara ya shule y sekondari ya wasichana
MWEDO kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Sayansi shuleni hapo Bw. Edickiel
Mturi.
Mwalimu
wa Taalum na msimamizi wa Maktaba wa Shule ya wasichana ya Mwedo,
Joseph Mangomes akiutambulisha ugeni wa UNESCO kwa wanafunzi na walimu
wa shule ya sekondari ya wasichana MWEDO wakati wa hafla ya kukabidhi
msaada wa vitabu shuleni hapo.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph,
akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MWEDO
wakati wa halfa ya kukabidhi vitabu vilivyotolewa na Shirika la Read
International kupitia UNESCO ambao aliwaasa wanafunzi hao kusoma kwa
bidii kuweza kukomboa familia zaidi hapo baadae kupitia elimu.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph
akionyesha baadhi ya vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na
Shirika la Read International kupitia UNESCO. Kulia ni Afisa Miradi
Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph,
akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi kwa
Mwanafunzi Evaline Gerald wa kidato cha pili shule ya sekondari ya
wasichana MWEDO uliotolewa na Shirika la Read International kupitia
UNESCO. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi
kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko (kulia) na kushoto ni
Afisa Mradi wa Shirika la Wanawake wa Kimasai (MWEDO) liliojenga shule
hiyo, Martha Sengeruan.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph,
Walimu na Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara
baada ya kukabidhiwa msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi
vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MWEDO wakishusha
maboksi yaliyosheheni vitabu vya masomo ya sanyansi vilivyotolewa na
Shirika la Read International kupitia UNESCO.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia