Wakongwe wa Klabu ya Real Madrid
ya nchini Hispania wakipiga picha za kikundi cha ngoma kilichokuwa
kikiwatumbuiza mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kabla
ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza
mara baada ya kuwasili kwa wachezaji wastaafu wa Klabu ya Real Madrid
kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
Meneja Mawasiliano wa TANAPA
Pascal Shelutete akigawa fulana maalum zenye nembo ya TANAPA na Real
Madrid kwa mmoja wa wachezaji kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro
Erastus Lufungulo akitoa neno la ukaribisho kwa wachezaji wastaafu wa
Klabu ya Real Madrid walipowasili kwa ziara fupi. Wengine katika picha
kutoka kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk.
Fenela Mukangara, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Elinas Palangyo, Kaimu
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Bi. Devota Mdachi, Meneja Mawasiliano wa
TANAPA Pascal Shelutete na Afisa Utalii Antipas Mgungusi.
Wachezaji wastaafu wa Klabu ya
Real Madrid pamoja na wenzi wao wakiwa Hifadhi ya Kilimanjaro.
Meneja Mawasiliano wa TANAPA
Pascal Shelutete (mwenye fulana nyeupe na miwani) akiongoza msafara wa
wakongwe wa Real Madrid kukwea Mlima Kilimanjaro
Wakongwe wa Real Madrid wakiwa katikati ya msitu wa Mlima Kilimanjaro
Eneo la Maporomoko ya Maji
ambapo wachezaji wakongwe wa Real Madrid walifanikiwa kufika Mlimani
Kilimanjaro.
Waziri wa Habari, Vijana
Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara akitoa cheti cha ushiriki kwa
mchezaji Ruben De La Red wa Klabu ya Real Madrid mara baada ya kumaliza
zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Wachezaji wakongwe wa Klabu ya
Real Madrid wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa TANAPA mara
baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia