Moto
Mkubwa ukiendelea kuwaka katika eneo la juu la Jengo la Shule ya
Sekondari ya Kiislam ya Mivumoni (Mivumoni Islamic Seminary) iliyopo
ndani ya Msikiti wa Mtambani,Kinondoni B Jijini Dar es Salaam leo.
Eneo
hilo ambalo lilikuwa likitumika kama Mabweni ya Wanafunzi wa Shule
hiyo,Maabara na Ofisi za Walimu limeteketea kabisa kiasi kwamba hakuna
kitu chochote kilichoweza kuokolewa.
Jitihada
za kuuzima moto huo zimekuwa zikiendelea hadi hivi sasa,huku sehemu ya
Waumini wa Kiislam wakijitokeza kwa wingi kusaidia juhudi hizo za
kuuzima moto huo zilizokuwa zikiendesha na Kampuni ya Kuzima moto ya
Ultimate,japo baadae gari hilo liliisha maji,hali iliyowapelekea Waumini
hao kulijaza maji gari hilo kwa kutumia ndoo huku kazi ya Uzimaji moto
huo ikiendelea.
Chanzo
cha Moto huo,inadaiwa ni hitilafu ya Umeme iliyokuwepo kwenye Bweni la
Wasichana Wanafunzi wa Shule hiyo.Hakuna mtu yeyote aliepoteza maisha
wala kujeruhiwa katika tukio hilo.
Moto mkubwa ukiendelea kuwaka kwenye eneo hilo.
Ulinzi mkali wa Polisi ulitawala katika eneo la Msikiti huo wa Mtambani kuhakikisha Usalama unakuwepo kwenye eneo hilo.
Sehemu ya Waumini wa Kiislam wakishirikiana kusombelea maji ili kuuzima moto huo