Banda
la Mtandao wa mashirika yapatayo 30 ya kupambana na matumizi ya kupita
kiasi ya pombe nchini (Tanzania Network Against Alcohol Abuse) kwenye
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani.
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI
imeshauriwa kutunga sera madhubuti ya udhibiti wa pombe katika jamii
ili pamoja na mambo mengine kuhakikisha vijana wanalindwa dhidi ya
bidhaa hiyo kwenye soko.
Akizungumza
na Moblog Tanzania jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo kikuu
wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana, Msemaji wa Mtandao
wa kupambana matumizi ya pombe kupita kiasi (Tanzania Network Against
Alcohol Abuse) Bw, Mathias Kimiro amesema kwamba kuna umuhimu wa
serikali kutunga sera mpya ya pombe ili kuzuia madhara kwa vijana na
taifa kwa ujumla.
“Kwa
kawaida matumizi ya pombe kupita kiasi ina madhara makubwa katika afya
ya mtumiaji lakini vile vile ina madhara kwenye familia kupitia kaya
moja moja na kusababisha mateso kwa familia hasa watoto,” amesema Bw
Kimiro
Amesema
kwamba umuhimu wa kuwa na sera madhubuti ya kudhibiti pombe katika
jamii ni kuangalia upya ni kwa kiwango ngani matangazo ya pombe
yanavyohamasisha unywaji kupita kiasi kwenye jamii.
Bw
Kimiro aliongeza kwamba mashirika yasiyo ya kiserikali yataendelea
kuwakumbusha mamlaka zinazohusika umuhimu wa kuwa na sera ya kudhibiti
pombe katika jamii pamoja na kuangalia madhara ya matangazo kwa wasomaji
wa mabango.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Makangarale Youth Theatre, ambao ni taasisi chini ya
Tanzania Network Against Alcohol Abuse (TAAnet), Bw. Ismael Mnikite
akifafanua jambo kwa Mgeni Rasmi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni,
Vijana na Michezo, Bibi Venerose Mtenga wakati wa maadhimisho hayo.
Aliongeza
kwamba sera ya pombe ni muhimu katika kuwabana makampuni ya vileo
kupunguza uhamasishaji wa unywaji wa pombe kwa sababu ina madhara
makubwa kwa vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa.
Bw
Kimiro amesema kwamba sera ya udhibiti wa pombe ikifanikiwa nchini
itapata fursa kupitia bunge kutunga sheria dhidi ya uuzaji na usambazaji
holela wa pombe kwenye jamii ya kitanzania.
Amesema
kwamba lengo la shirika lao ni kuhamasisha uwepo wa sera ya pombe
nchini Tanzania kwa sababu hakuna sera mbali kuna sheria ndogo ndogo
zilizowekwa katika jamii.
Bw
Kimiro alifafanua kwamba hata sheria hizo ndogo ndogo siku hizi
hazitekelezwi kama vile muda wa kuuza na kutokuuza pombe hauzingatiwi
nah ii kupelekea upatikanaji wa pombe kiholela kwenye jamii.
Amesema
kwamba ina madhara mengi kwa mfano kijamii unyanyasaji wa kijinsia hasa
kwa wanawake na watoto na ndoa nyingi huvunjia na baadhi ya wanawake
kubakwa na watoto kukosa mahitaji muhimu.
Bw
Kimiro aliongeza kwamba madhara ya pombe kiuchumi ni makubwa kama vile
kupunguza nguvu kazi ya taifa, matumizi mabaya ya fedha na kusababisha
njaa kwenye jamii baada ya nafaka nyingi kutumiak kutengeneza pombe.
Shirika
la Tanzania Network Against Alcohol Abuse ni mtandao wa mashirika
yapatayo 30 ni ilianza kazi rasmi mwaka 2011 na ina matawi Dar es
Salaam, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.
Mgeni
rasmi akipata maelezo kutoka kwenye banda la Tanzania Network Against
Alcohol Abuse kwenye moja la shirika lake la Tanzania Girl Guides
Association, anayetoa maelezo ni Fadhia Khamis Ally na kushoto kwake ni
Shadya Soud Milanzi wasichana hao wanatoka Girl Guides ambacho ni chama
kisicho cha kiserikali na ni chama cha kujitolea, madhumuni yake ni
kuwaendeleza wanawake pamoja na mtoto wa kike katika maswala ya kijamii
na kiuchumi kwa kuwapa elimu na mafunzo.
Msemaji
wa Mtandao wa Kupambana na matumizi ya kupita kiasi ya pombe, Tanzania
Network Against Alcohol Abuse, Mathias Kimiro akizungumza na Moblog
Tanzania umuhimu wa serikali kuja na sera na baadaye sheria ya kudhibiti
pombe nchini wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana
duniani.
Baadhi
ya wafanyakazi kutoka mashirika mbalimbali chini ya Mtandao wa
kupambana na matumizi ya pombe, Tanzania Network Against Alcohol Abuse
wakiwa katika picha ya pamoja kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya
vijana duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam.