WAREMBO 17 KUCHUANA REDS MISS NORTHERN ZONE
Jumla ya
warembo 17 wanaoshiriki shindano la Reds Miss Northern Zone wanataraji kuchuana
vikali mnamo julai 5 mwaka huu kwa lengo la kumpata mrembo atakayeiwakilisha kanda hiyo katika shidano la Miss Tanzania.
Warembo hao
wanataraji kuingia kambini juni 28 mwaka huu katika ukumbi wa Triple A ambapo
watakuwa chini ya walimu Zakhia Ramadhan ,Angel Justaz na Joseph Mgani.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa kampuni ya Mwandago Investment Entertainment,Faustine
Mwandago ambaye ndiyo mwandaaji wa shindano hilo alisema kuwa warembo kutoka
jijini Tanga tayari wameshatinga Arusha .
Alisema kuwa
katika shindano hilo warembo kutoka mkoani Manyara wako watano,Kilimanjaro wako
4,Tanga wanawakilishwa na warembo 3 na mwenyeji Arusha inawakilishwa na warembo
5.
Mwandago,alisisitiza
ya kwamba mwaka huu shindano hilo litanogeshwa na bendi ya F M Academia kutoka
jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni mbunge wa viti
maalumu mkoani Arusha,Catherine Magige(CCM).
Hatahivyo,alisema
kwamba mwaka huu wamejipanga katika suala la hali ya hewa ambapo kutakuwa na
majiko ya moto ya kisasa kwa ajili ya kukabiliana na hali ya hewa ya baridi
ukumbini huku upande wa ulinzi kutakuwa na ulinzi mkali nje na ndani ukiongozwa
na mbwa wakali watakaokuwa wameambatana na askari kutoka kampuni ya ulinzi wa
Geo Security.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia