WAZEE WILAYA YA ARUSHA WAMUOMBA RASI MAGUFULI NAFASI MOJA YA UWAKILISHI BUNGENI KATIKA NAFASI ZAKE KUMI

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Gabriel Daqarro wakitoa Maagizo kwa watendaji wa serikali na taasisi kuwapa kipaumbele cha kwanza wazee wakati akiongea

Katikati Ni mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro na kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Arusha David Mwaiposa na kushoto ni mwenyekiti wa baraza la wazee wilaya Arusha Mhina Sezua wakati wa mkutano na mkuu huyo wa wilaya kubaini changamto mbali mbali wanazokumbana nazo wazee wilayani hapa

Meza kuu wakifuatilia hoja mbali mbali zilizokuwa zinatolewa na wazee leo jijini Arusha

Sehemu ya wazee waliohudhuria mkutano huo wakiwa wanamsikiliza mkuu wa wilaya Gabriel Daqarro

Katibu wa wazee akiongea katika mkutano huo

WAALIMU WASTAAFU NAO HAWAKUWA NYUMA KWENYE KIKAO HICHO

Katibu Tawala wilaya ya Arusha David Mwaiposa akiwa anamkaribisha mkuu wa wilaya kuongea na wazee ilikujua kero zinazowakabili

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akiongea na wazee wa jiji la Arusha ambao wamemuomba mkuu huyo kuwafikishia salamu zao kwa viongozi wakuu wa serikali akiwemo raisi dkta John Magufuli kuwa wakifika Arusha waweze kuonana na baraza la wazee kama wanavyoonana na wazee wa Dar es salaam

Mwakilishi wa OCD nae akijibu maswali ambali mbali kwa niaba ya mkuu wa polisi wilaya ya Arusha

Mwenyekiti wa baraza la Wazee wilaya ya Arusha mjini Mhina Sezue akiongea katika mkutano huo ambao aliiomba serikali wilayani hapa kuwapa uwakilishi wazee kwenye mabaraza ya serikali kuanzia ngazi ya kijiji kata hadi Taifa huku wakimuomba raisi kuwapa nafasi moja katika zile kumi za uwakilishi wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Hata sisi hatupo nyuma kama walivyokutwa na kamera wakiingia ndani ya ukumbi wa Simba kwenye kituo cha mikutano cha AICC Leo Jijini Arusha

WAZEE HAWA NAO WALIKUWEPO KATIKA KUTOA MICHANGO YAO YA MAWAZO KUBORESHA HUDUMA ZAO

wakifuatilia mkutano huo kwa umakini

Bibi akifuatilia mkutano huo wa mkuu wa wilaya ya Arusha na wazee wa jiji la Arusha leo jijini Arusha

Sehemu ya wakifuatilia mkutano huo

Mandari ya muitikio wa wazee kwenye mkutano huo wakiwa katika ukumbi wa simba hall

wazee wakifuatilia mkutano huo kwa umakini na kueleza kero mbali mbali kwa mkuu wa wilaya ya Arusha

WAALIMU WASTAAFU NAO HAWAKUWA NYUMA KAMA HAPA WAKIFUTILIA MKUTANO HUO.Picha zote na mahmoud ahmad arusha
MKUU wa wilaya ya Arusha, Gabriel Fabian Daqarro, amemugiza afisa Usitawi wa jamii wa halmashauri ya jiji la  Arusha kuhakikisha wazee wote wa jiji hilo wanapatiwa vitambulisho kabla ya mwisho wa mwaka huu ili waweze kupata huduma mbalimbali ikiwemo matibabu kwenye  Hospitalini mbalimbali.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo jana kwenye mkutano na wazee wa jiji la Arusha uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa ,AICC, ulikuwa una lengo la kusikiliza kero za wazee ili zipatiwe ufumbuzi pia kufahamiana.

Mkuu huyo wa wilaya ameiagiza Idara hiyo kuhakikisha vitambulisho vinapatikana kabla ya mwisho wa mwezi, sanjari na kuwataka watendaji wa serikali, mashirika ya umma na taasisi mbali mbali za serikali katika jiji la Arusha kuhakikisha kuwa zinatoa kipaumbele kwa wazee ambao wamekuwa hawapati huduma zao kwa wakati.

Aidha amewataka wenyeviti wa mitaa,kata na tarafa kushirikiana na jeshi la  na jeshi la polisi kuhakikisha wanaimarisha usalama kwenye maeneo yao ili kuwezesha wazee kuishi kwa usalama bila kubughudhiwa na kuhakikisha wanasiamia maadili.

‘’Mumepewa madaraka ya kuimarisha ulinzi yatumieni ili wazee wasibughudhiwe ,tambueni kuwa wazee ni muhimu ndio waliotufikisha hapa sasa sitaki kusikia kuwa wanasumbuliwa sitaki kusikia malalamiko ya ya kuporomoka kwa maadili ””alisema Daqarrro.Wakichangia  kwenye mkutano huo wazee wamedai kuwa taasisi za fedha pamoja na halmashauri ya jiji haziko tayari kuwakopesha wazee kwa hofu ya kuwa watakufa karibuni na  kutaka dhana hiyo iondoke kwa kuwa kuzeeka sio kufa .

Wamesema nao wana mahitaji mbalimbali ya kuendesha sghuhuli zao za kiuchumi hivyo wanayo haki ya kupewa mikopo kama yalivyo makundi mengine ya jamii.

Wameomba kushirikishwa kuanzia ngazi ya mtaa hadi halmashauri ili wawe na wawakilishi wao ambao watawasilisdha kero zao kwenye vikao vya maamuzi vya serikali na baraza la madiwani pia wapate uwakilishi bungeni kama yalivyo makundi mengine ya walemavu, vijana na wanawake.

Wamelalamikia kukosa Vitambulisho ambavyo vingeliwawezesha kupata huduma za haraka kwenye taasisi mbalimbali za serikali,ikiwemo dawa kwenye hospital za serikali, pia wamelalamikia lugha za kuwadharirisha zinazotolewa na baadhi ya wahudumu wa hospital za serikali na vituo vya afya.Wamelalamikia hatua ya Zahanati kutokutoa huduma siku za mwisho wa wiki hali ambayo inawasababisha kukosa huduma za matibabu.Aidha wamelalamikia TASAF kutoa fedha kwa ajili ya watu wasiokuwa na uwezo kwa upendeleo ambapo walengwa wamekuwa hawanufaiki na mpango huo wa TASAF.

\

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia