BREAKING NEWS

Saturday, April 27, 2013

CHADEMA KUMFIKISHA MAHAKAMANI MKUU WA MKOA WA ARUSHA DHIDI YA KAULI ZAKE ZA UCHOCHEZI


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo mkoa wa Arusha(CHADEMA)kimesema kuwa
kinatarajia kumfungulia mashitaka mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa
Mulongo dhidi ya kauli zake za uchochezi  dhidi ya Chama hicho  lakini
pia kauli za vitisho kwa Mbunge Lema ambaye kwa sasa anashikiliwa na
Polisi.

Akizungumza na vyombo vya habari mapema jana Katibu wa chama hicho
Amani Golugwa alisema kuwa zoezi hilo lipo mbioni kukamilika kwa kuwa
wanasheria wa chama hicho tayari wameshapewa taarifa hizo

Golugwa alisema kuwa Magesa Mulongo amekuwa kikwazo kikubwa sana kwa
kuwa sio mara ya kwanza kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Chadema
lakini hata mara nyingine amekuwa akimtuhu Lema kwa uongo uongo hali
ambayo hadi kwenye mauaji ya chuo cha uasibu ilijitokeza

Aliendele akwa kusema kuwa kama wataweza kupuuzia hali hiyo itazidi
kuwaumiza sana na ikubambikiwa kesi ambazo si za kwao kama hali ilivyo
kwa sasa ambapo kuna dalili za Mbunge Lema kubambiwa kesi ya mauaji
yaliyotokea katiika chuo cha Uasibu

“tunavyoongea mpaka sasa tayari tumeshawasiliana na wenzetu ambao ni
wanasheria wa Chadema na tutamfikisha mahakamani huyu Mkuu ili iwe
fundisho kubwa sana manake kauli zake za uchochezi na za kutupinga
sisi zinatuchosha sana na mimi kama Katibu naona amefilisika kisera na
hata kimawazo kwa kuwa kamwe siwezi mfananisha hata na mtendaji wangu
wa chama”aliongeza Golugwa

Akiongelea Kesi inayomkabili Mbunge Lema alisema kuwa mpaka sasa
mlalamikaji katika kesi hiyo hakuna lakini vitisho alivyotoa mkuu huyo
wa mkoa vinasema kuwa Lema kwa sasa hatabanduka na wala hatachomoka
hali ambayo ni fedheha tu lakini wao kupitia kwa mwanasheria wao
wanajopanga vilivyo kukabiliana na Mkuu huyo wa mkoa

Awali Wakili wa Mbunge Lema ambaye ni Bw Humprey Mtui alisema kuwa
anashangazwa na kitendo cha jeshi la polisi kumvunjia hesima mbunge
Lema na badala yake kumfanya kama Kapurwa mtaani kwa shinikizo la
maslahi ya watu wacheche

Alisema kuwa kwa mujibu wa sheria Lema angepswa kuitwa na Polisi
lakini kama angetaa basi ndio angeweza kuchukuliwa sheria kama hiyo
lakini sio kwa kitendo cha polisi walichokifanya cha kuvuka ukuta wa
nyumba ya mbunge huyo

Bw Mtui alisema kuwa mbali na hayo pia hata haki za msingi kama vile
kuswaki na kunywa chai mbunge huyo ananyimwa na Polisi jambo ambalo ni
ukiukaji mkubwa sana wa Sheria ya Maabusu hapa Nchini ukilinganisha
kuwa yeye bado ni mbunge na tena mwakilishi wa wananchi

Alifafanua kuwa bado watakuwa na mbunge huyo na wataweza kufuata
sheria za msingi lakinii kwa wale wote ambao wanamuonea Mbunge huyo
watachukuliwa sheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani kwani
hali za uoneaji dhdi yake zinaongezeka siku hadi siku.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates