WAZIRI Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika mbio za Sokoine Marathon, zinatakazofanyika, Aprili 12, mwaka huu, wilayani Monduli, mkoani Arusha.
Edward N. Lowassa |
Akithibitisha hilo Mratibu wa mbio za Sokoine Marathon 2013, Bw. Wilhelm Gidabuday aliiambia TAIFA LETU.com kuwa tayari wameshapata uthibitisha wa kuwepo kwa kiongozi huyo akiongozana na viongozi wengine wakuu wa nchi wakiwemo Mawaziri na Wabunge.
“Kutokana na wadhifa na heshima aliyokuwa nayo Marehemu Sokoine tumeona ni vizuri kuwaalika viongozi wetu wakuu wa nchi,na watu wengi tu watakuwepo, wabunge, mawaziri wakiongozwa na mheshimiwa Lowassa, wananchi wa kada mbalimbali, lengo ni kumpa heshima inayostahili kiongozi wetu,” alisema Gidabuday.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya maandalizi aliyepewa jukumu la kuwasiliana na viongozi ikiwa ni pamoja na Mgeni Rasmi, Mbunge wa viti maalum jimbo la monduli (CCM), Namelok Sokoine alisema kuwa, tayari wameshapata uhakika wa uwepo wa Lowassa katika mbio hizo.
Sokoine |
Akizungumzia swala la kutoa namba pamoja na usajili, Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Arusha (ARAA), Joseph Jorwa alisema tayari utaratibu wa kuandaa namba umeshakamilika na kuongeza kuwa zoezi la usajili utafanyika baada ya siku kuu za Pasaka, katika Ofisi za ARAA, zilizoko katika uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kwa ada ya sh. 2000 za Tanzania.
Sokoine Marathon zitahusisha mbio za kilometa 10 na kilometa 2 kutembea na kukimbia na zitatanguliwa na misa maalum zitakazofanyika katika kanisa la katoliki alililokuwa ni muumini kijijini kwake na zinatarajia kukutanisha watu mbalimbali kumuombea kiongozi huyo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia