MWALIMU AFARIKI NA AJALINYA PIKIPIKI
Mwalimu wa
shule ya sekondari Musa afa kwenye ajali ya pikipiki eneo la kisongo nje kidogo
ya jiji la Arusha wakati akiendesha pikipiki yake aina ya Honda yenye namba za
usajili T164BAA baada ya kugongwa na gari huko kisongo.
Akizungumza
na vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoani hapa kamishna msaidizi wa polisi
Liberatus Sabas alisema kuwa Mnamo majira ya usiku huko maeneo ya kisongo
barabara ya Dodoma gari lenye namba za usajili T647AQH aina ya RAV4 iliyokuwa
ikiendeshwa na Lambert Teuwissen miaka32 raia wa Holland mkazi wa moshono
alimgonga mwendesha pikipiki na kusababisha mauti ya mtu huyo.
Kamanda
Sabas alisema kuwa mtu huyo alitambuliwa kuwa ni mwalimu wa shule ya sekondari
musa aliyopo kisongo na katika hatua nyingine siku hiyo hiyo huko maeneo ya
Ilbouru gari namba T231CAR aina ya TOYOTA hiece iliyokuwa ikiendeshwa na dereva
asiyefahamika ilimgonga mwendehsa piki piki na kusababisha mauti wa abiria wa
pikipiki hiyo.
Pikipiki
hiyo yenye usajili no.T138CBJ iliyokuwa ikiendeshwa na Sadiki Athman miaka 20 ilipata
ajali na kusababisha kifo cha Maliki Bakari(23)ambaye alikuwa abiria wa
pikipiki hiyo huku dereva akipata majeraha sehemu mbali mbali za mwili wake.
Kamda Sabas
alisema kuwa anatoa wito kwa madereva wanaoendesha vyombo vya moto na vya
usafiri kuchukuwa tahadhari na kuwa makini kwa kuzingatia kanuni na sheria za
usalama barabarani ilikuepuka matukio ya ajili .
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia