Sehemu
ya Wamiliki wa Blogs mbali mbali hapa nchini wakiwa kwenye picha ya
pamoja na Mgeni Rasmi katika hafla maalum ya mwaka kwa Tanzania Bloggers
Network,ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT),Ndg.
Kajubi Mukajanga pamoja na baadhi ya wadhamini waliofanikisha hafla
hiyo,iliyofanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es
salaam.
Mgeni
Rasmi katika hafla maalum ya mwaka kwa Tanzania Bloggers Network,Katibu
Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT),Ndg. Kajubi Mukajanga (wa pili
kulia) akizungumza jambo na baadhi ya Wamiliki wa Blogs
Tanzania,waliokutana pamoja leo kwa lengo la kufahamina na kuunganisha
vyema umoja wao.
Mkurugenzi
wa Masoko kwa Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania ambao ndio walikuwa
wadhamini wakuu,Kelvin Twissa akizungumza machache katika hafla hiyo.
Mkongwe
kwa maswala ya kublog hapa nchini,Ankal Issa Michuzi akifafanua jambo
kwa baadhi ya wageni waalikwa juu ya kukutana kwao kwenye hafla hilo
iliyofanyika usiku huu kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja kwa baadhi ya Wanablog na wadhamini wa hafla hiyo.