Raisi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu Jaji Agustino Ramadhani
Akihutubia mkutano wa Haki za binadamu uliofanyika jana jijini Arusha
lengo la kuimarisha haki za binadamu na kushirikisha taasisi binafsi na za
serikali katika kuisaidia Mahakama hiyo

amesema kuwa lugha ya Kiswahili itaanza kutumika katika mahakama hiyo ili
kuwawezesha watu kusoma na kuelewa taarifa muhimu zinazotolewa
zitakazowawezesha
kujua na kuimarisha haki hizo za msingi kwa kila mmoja
.
Jaji Agustino Ramadhani amesema kuwa lugha ya Kiswahili inazungumzwa na
nchi nyingi barani Afrika hivyo umefika wakati wa kubadilisha taarifa na
nyaraka mbali mbali kutoka lugha za kigeni na kuwa katika Kiswahili ili
kukuza uelewa wa watu juu ya haki za binadamu.
Raisi huyo ameeleza hayo katika mkutano wa haki za binadamu ulioandaliwa na
Mahakama hiyo kwa kushirikiana na Mashirika na taasisi binafsi
zinazojihusisha na haki za binadamu uliofanyika jijini Arusha
jana,Ramadhani amesema kuwa mashirika binafsi yana nafasi kubwa ya kutoa
elimu kwa wananchi na kuhamasisha uzingatiaji wa haki hizo.
Mwenyekiti wa Mashirika binafsi yanayotetea haki za binadamu na kufanya
kazi kuisaidia mahakama hiyo George Kisoro amesema kuwa suala la
kuanzishwa kwa mahakama ya Afrika ya Makosa ya jinai kwa mujibu wa mkataba
wa Malabo unaojulikana kama Malabo Protocol na kupitishwa Juni 2014 bado
una kasoro mojawapo ni kuwepo kwa kifungu ambacho hakiruhusu rahisi
kushitakiwa akiwa katika kipindi cha uongozi wake.
"Kifungu hichi kitawafanya viongozi wa Afrika kung`ang`ania madaraka kwa
kuogopa kuwa iwapo wakiachia madaraka watashitakiwa katika mahakama hiyo
kwa upande mwingine ina madhaifu" Alisema George
George alisema kuwa kutokana na Viongozi wa Afrika kutorishiwa na mwenendo
wa Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai iliyoko the Heague
walipendekeza kuanzishwa kwa Mahakama ya Afrika ya makosa ya jinai
itakayoendesha makosa ya jinai yanayowakabili viongozi.
Anaeleza kuwa kwa sasa hali ya haki za binadamu kwa bara la Afrika bado ni
mbaya hasa katika maeneo yenye vita kama nchini Congo na Sudan ambako
vitendo vya kikatili na unyanyasaji wanafanyiwa wanawake na watoto ikiwemo
ubakaji,kukatwa viungo vya mwili,vipigo vikali .Katika maeneo hayo kuuana
imekua ni utamaduni wa kudumu suala ambalo si zuri.

Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia