Wafanyakazi wa kampuni ya
Tan Communication Media inayo miliki kituo cha Radio 5 chenye makao
yake makuu jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja jana katika mafunzo ya
kuwajengea uwezo wa kitaaluma ili waweze kuandika habari za kuboresha
maisha ya jamii kwa kupata maendeleo kuelekea uchaguzi mkuu,mafunzo hayo
yanaendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la BBC Media Action,
aliyevalia shati la blue ni mkufunzi mwandamizi Pendael Omari wa shirika
hilo
Mkufunzi
mwandamizi Pendael Omari wa shirika lisilo la kiserikali la BBC Media
Action akiwa anatoa ufafanuzi katika mafunzo hayo yaliyokuwa yakifanyika
katika ofisi za Radio 5,mafunzo hayo yalidumu kwa takribani wiki mbili
Mtangazaji
maarufu wa kituo hicho Ernest Matundiro a.k.a Prince de la ville
kushoto akiwa anaandika vipengele muhimu katika uandishi wa habari,kulia
ni Mhariri wa kituo hicho Monica Nangu
Msimamizi
mkuu wa vipindi vya Radio 5 kulia Mathew Philip akiwa anafatilia
mafunzo kwa ukaribu zaidia,kushoto ni mtangazaji wa kituo hicho Wilberd
Kiwale
Wafanyakazi wa Radio 5 jijini A rusha wamepatiwa mafunzo ya
kuwajengea uwezo wa kitaaluma ili waweze kuandika habari za kuboresha
maisha ya jamii kwa kupata maendeleo kuelekea uchaguzi mkuu,mafunzo hayo
yanaendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la BBC Media Action,
Akizungumza katika mafunzo hayo Mkufunzi
mwandamizi Pendael Omari wa shirika lisilo la kiserikali la BBC Media
Action alisema kuwa lengo la kufanya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa
kitaaluma pindi wanapokuwa katika kazi zao
Alisema
kuwa mafunzo hayo yatawezesha pia upatikanaji wa utawala bora kwa kuwa
vyombo vya habari vitaelimisha wananchi umuhimu wa kuchagua viongozi
watakaoleta maendeleo
Kwa upande wake Msimamizi mkuu wa vipindi vya radio hiyo
Mathew Philip alisema kuwa mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kufanya
kazi kwa kuwa walikuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo zaidi
Pia
alisema kuwa kupitia mafunzo hayo wamepata ufahamu wa namna ya kutafuta
habari za kupigia kura maoni pamoja na uchaguzi mkuu bila upendeleo kwa
kumpa msikilizaji nafasi ya kusikika na kumpa elimu
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia