Dear
Friends
Napenda kutoa taarifa kwamba kumekuwa na tapeli mmoja
ambae amekuwa akitumia picha zangu kwa kufungua facebook accounts kwa
majina mbali mbali kama Justin Stan,James Brown,Onesmo,Felister Julius,
Anthony Yohana au Yohana Anthony na mengineyo mengi.
Mtu
huyu amekuwa akijenga urafiki na watu wasiotambua kuwa ni TAPELI katika
mtandao wa kijamii wa Facebook
Urafiki ukiwa umekamilika kwa maana ya friends request
kutoka kwake and acceptance kutoka kwa victim amekuwa akiwaambia marafiki
zake hawa wa Facebook kuwa yeye ni muajiriwa sehemu mbali mbali tofauti
katika kila account hizi za facebook kama kwa mfano kwingine akidai
anafanya Vodacom Mlimani City, kwingine akidai anafanya Tanesco Makao
Makuu,PPF na sehemu nyingine kadhaa na amekuwa akiwaahidi kwamba ana watu
wenye uwezo wa kuwaunganishia kazi sehemu hizo kwa sharti la wanaotaka kazi
kujikusanya na kufikia idadi ya watu watano na wakilipa kiasi cha shilingi
50,000 kila mmoja basi watapata nafasi za kazi hizo.
Wakati
mwingine amekuwa akiwa wadanganya baadhi ya watu kuwa yupo mkoani kikazi au
akihudhuria semina na kwamba mdogo wake anashida ya dharura ya pesa kama
shilingi 25,000 au 30,000 na kuomba marafiki wamtumie na kuwaahidi
atawarudishia mara atakapokua free, amekuwa akitoa namba mbali mbali za
simu mojawapo zikiwa hizi 0785412653 na 0688081032. Wale walioshtuka
amekuwa akiwatukana matusi makubwa ya nguoni bila uoga.
Natoa
tahadhari kwa watu wote kujihadhari na kufanya urafiki na watu msio wajua,
kuzingatia umakini haswa katika mambo ya pesa, pia kujua watu wa namna hii
ni wengi sana online haswa kwenye social media. Nashauri uki suspect mtu wa
design hii basi wasiliana na polisi na ikibidi kumtengenezea mtego wa
kumnasa.
Vijana
tunatakiwa tuchape kazi kwa nguvu na sio kutafuta njia za mikato. Hakuna
hadithi yeyote niliyowahi kuisikia ya aliyefanikiwa katika maisha kwa njia
ya mkato. Mwana fundi ni kusoma kwa bidii ili elimu yako ikupatie
ajira.
Mwisho naomba marafiki zangu wooote mnisaidie kurepost message hii kwani
naamini itawaokoa wengi (vulnerable) ambao kwa namna moja au nyingine
wanaweza kuwa hawajui utapeli huu wa online.
Picha
hiyo hapo juu ni yangu na ndio amekuwa akiitumia kwenye account nyingi za
facebook.
Mimi
ninaamini Mungu na hivyo huyu bwana Siku zake 40 zipo karibu. Napenda pia
kwa namna ya kipekee nawashukuru wale wote (zaidi ya 10) waliotumia muda
wao kunitafuta na kunipa taarifa hizi muhimu walipomshtukia Tapeli
huyu.
Mwenyezi Mungu awabariki saana.